LAPF

LAPF
LAPF

Ijumaa, 8 Oktoba 2010

The Upanga Story - The Strokers

The Strokers, hili lilikuwa kundi jingine la wanamuziki wa Upanga. The Strokers lilikuwa na awamu mbili, ya kwanza ilikuwa na wanamuziki akina Donald Max, David Max, Harry Chopeta, Vincet Chopeta, Pino Makame na Ochiwa na Freddy Lukindo. Awamu ya pili ya kundi hili ilikuwa na Sajula Lukindo,Onesmo Kibira,Innocent Galinoma,Ben Galinoma, Denis Pad,Francis Kasambala,Vicent na Harry Chopeta, Ally Mwarabu, Sabri Mmanga na wengineo. Pichani ni awamu ya kwanza ya Strokers. Waliosimama, Pino Makame, Freddie Lukindo, David Max. Waliokaa (?),Harry Chopeta, Vincet Chotepa.

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

Ki ukweli blog hii ni superb. Inakila kitu cha kisasa kinachoifanya iwe ya kisasa bilamadoido mengi ya kishamba. Tujumuike kwa pamoja kuleta michango na kumbukumbu nyingi za furaha huzuni na zakale.
John hapo pembeni kwenye utambulisho wako umesema wewe ni mwanamuziki MUOMBAJI. Nadhani ulidhamiria kusema MUIMBAJI.

Bila jina alisema ...

John, kama unaweza kutumia contacts zako BASATA na BAMUTA, naomba uwaeleze kama wanaweza kufanya collection ya wasanii na wanamuziki wa zamani kwa maonyesho au hata kuweka kumbukumbu. Kama alivyosema Malcolm X "Watu wasioijua historia yao hawataweza kujielewa wala kujithamini wala kujipangia mstakabala wao".

Bila jina alisema ...

John Nimekukubali (ndio maana njenje inatufanya tusilale jumamosi) hapa nimemuona Vincent Chopeta alikuja kuwa mfamasia ingawa sijamuona siku nyingi

innocent Galinoma alisema ...

JK hii ni kumbukumbu nzuri sana. wakati huu mie nilikua bado sijajiunga na hili kundi la Les-Strokers. Tulikua darasa moja na Vincent Chopeta, Crispin Makame na Noel Chikoti shule ya msingi ya Muhimbili, Vincent ndio aliyenifundisha mimi kupiga gitaa na baadaye nukajiunga nao nikiwa kama mpiga ngoma,na awamu ya pili ya Les-Strokers tulia Harry na Vincent Chopeta, Fransis Kasambala,Ochiwa, Dennis, Bern na Innocent Galinoma, Sajula LukindoDavid maxi alihamia Bar-locks.nilipofika Minneapolis kwenye kusajili jina la bendi yangu ya Exodus nilikuta hilo jina limashawaiwa na The-Exodus pia kwa hivyo ndio nikachukua Les toka Strockers na kusajili kama Les-Exodus.
Asante sana JK kwa kutukumbusha ujanja wa utoto wetu.
Innocent Galinoma Mfalingundi.

John Mngodo alisema ...

Ni juzi tu (Siku tatu zilizopita) nilikutana na Harry Chopeta mtaani jijini Dar baada ya miaka mingi kupita. Sikujua kuwa huko nyuma pamoja na akina Freddy Lukindo, Ochiwa na wengi naye alikuwa ni wanamuziki. Baadhi niliwafahamu kama akina Onesmo Kibira na Innocent Galinoma ambao najua kuwa bado ni wanamuziki mahiri kule Marekani. Sisi wengine hatukujua kingine zaidi ya kujikita katika soka la mchangani. Baada ya mazungumzo mafupi na Harry tukikumbushana ya enzi zile za Upanga tukiwa pale Mtaa wa Jamhuri hapo ndipo nilikuja kufahamu kuwa kumbe yule ndogo wake yaani Vincent sasa ni marehemu. Sasa yapata miaka mitatu hivi. Kati ya wale walioko kwenye picha nafahamu mwingine pia ni marehemu. Mungu aziweke Roho zao mahali pema. All in all thanks John Kitine Kwa kumukumbu hizo nzuri. - John Mngodo