LAPF

LAPF
LAPF

Ijumaa, 1 Oktoba 2010

Vijana Jazz enzi za Ngapulila


Kati ya awamu nyingi za Vijana Jazz Band moja iliyoleta changamoto na furaha ni ile awamu ya nyimbo , Ngapulila, Ogopa Tapeli, Adza. Pichani baadhi wa wanamuziki wa wakati huo. Picha ya kwanz a juu- Mzee Joseph Nyerere akiwa na Kulwa Milonge na Hamis Mnyupe, picha ya pili wapiga trumpet marehemu Chondoma, Hamis Mnyupe, na Kulwa Milonge. Picha ya chini ni kundi zima la Vijana Jazz wakiwa na Mheshmiwa Seif Khatib, hapa wanaonekana akina Shaaban Dogodogo, Hemed Maneti,Shaaban Wanted, Abou Semhando na wengine wengi.Kama unavyoona alama za x wengi hawapo tena nasi duniani.Maoni 1 :

Abu alisema ...

kaka asante kwa dokezo hili fupi. yawezekana ukatupa habari zaidi juu ya stori hii, maana umegusa tu ukatuacha tunaning'inia. nyimbo zipi zilitamba, zilitungwa na kuimbwa na akina nani, waliotutoka (mungu awarehemu) ni akina nani, nk nk