LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 12 Desemba 2010

Dr Remmy Ongala hatunae tenaMwanamuziki wa siku nyingi ambaye aliepitia bendi ya Orchestra Makassy, Super Matimila, na hatimae kumalizia maisha yake akimwimbia Mungu kupitia nyimbo za enjili hatunae tena. Amefariki jana tarehe 12 Desemba 2010, saa sita usiku katika hospital ya Regency mjini Dar. Siku za karibuni Remmy alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akiwa nasumbuliwa na kisukari na matatizo ya figo, na akawa ameruhusiwa na kurudi nyumbani, na alipozidiwa jana  akapelekwa Regency ambapo mauti yalimkuta. Mazishi yanasubiri binti zake ambao wako nje ya nchi. 
MUNGU AMLAZE PEMA REMMY ONGALA

Hakuna maoni: