LAPF

LAPF
LAPF

Jumatano, 15 Desemba 2010

Mkesha wa mazishi ya marehemu Remmy Ongala


Kweli huu ulikuwa mkesha wa kumuaga mwanamuziki nguli. Nje ya nyumba ya DR Remmy, pale Sinza, kulipangwa seti mbili ya vyombo vya Bendi na seti ya Disco. Disco ambalo limekuwa likiendelea toka  jana lilikuwa usiku na mchana likipiga nyimbo mbalimbali za marehemu Remmy Ongala wakati akiwa na Super Matimila. Usiku huu wanamuziki mbalimbali walipanda kwenye stage wakaimba na kupiga nyimbo zao na za bendi ya Super Matimila pia. Kasaloo Kyanga alikuwepo na kukumbusha nyimbo za enzi ya Super Matimila ambapo waimbaji walikuwa yeye Kasaloo, Skassy Kasambula, na marehemu. Wanamuziki wa kizazi kipya kama Bushoke Jnr nao walipanda na kuimba nyimbo zao. Wanamuziki wa zamani kama Kadesi, Nkulu wa Bangoi,nao walionekana baada ya kupotea machoni kwa watu kwa miaka mingi. Ulikuwa mkesha uliostahili mwanamuziki kama Dr Remmy
Kadesi mpiga bass wa zamani wa OSS

Kasaloo Kyanga

Watu katika onyesho la mkesha

Mafumu Bilali Bombenga'Super Sax'
Mtoto wa Chinyama Chiyaza


Mwema Mudjanga, Nkulu Wabangoi, na Kabeya Badu

Makassy Jnr na Mzee Mwema

Mzee KungubayaBushoke Jnr katika shati la chui

Mafumu

Malu Stonch

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

One of the greatest musicians to ever graced the once respectable country Tanzania. Walioziona hizi enzi wakiwa na umri mkubwa wanasema “that was early 80s when economy was still sound, everyone was looking forward to weekend in Dar. Good old days” How I wish I were there! Rest in peace MAESTRO DR ONGALA. By the way this man is more deserving to be honoured with a PhD than Jk, Makongoro, Nagu, Nchimbi and other crooks in the current government.

Kisondella, A.A alisema ...

Mzee Kitime,

Kwanza nimesikitishwa sana na Kifo cha mwanamuziki wa muda mrefu, Dr. Remmy. Mwanamuziki ambaye alitumia muda mrefu kutunga na kuimba nyimbo zake zikiwa katika mtizamo wa watu wa chini, wenye kipato kidogo, wanyoge.

Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya wanamuziki kwa dansi Tanzania nikishuhudia jinsi wanamuziki wetu wanavyotakiwa kuagwa, hiki ndicho nillikuwa nakitafuta muda wote, sijui nani kavumbuka na kuandaaa haya yote. Imekuwa jambo lakusikitisha wanamuziki wetu ambao tumekuwa tukifurahia kazi zao wanazikwa kimya kimya na wakati mwingine unashangazwa kusikia mwanamuziki fulani alifariki.

Ningependa wadau wote wa muziki wetu wa dansi na pia wasanii wa anga nyingine tuwaenzi pale wawapo hai na pia wanapotutoka.

Mfano ya msiba ambayo wanamuziki wake walifariki lakini sikuona heka heka kama za msiba wa Dr. Remmy ni Athumani Momba, Joseph Mahina, Tx Moshi William, Sulemain Mbwebwe, Muhidini Kisukari, Kassim Mponda,(Msondo), King Enock, Machaku Salum, Suleiman Mwanyiro, Chipembele Said, Gervas Helman, Adam bakari, Fransis Lubua, Hamisi Juma, Kassim Rashid, n.k (Sikinde), na wengineo wengi ambo sijawataja, Hakika mazishi yao nafiri kama si wanamuziki wenza pamoja na majirani sidhani kama kuna watu walienzi kama nionavyo wa Dr. Remmy.

Wanamuziki Tubadilike!!!

Roho yake Dr. Remmy iwekwe mahali pema peponi, Tutakukukosa kimwili, lakini miziki yako tutienzi Daima

Kisondella - (Mafinga-Iringa)

Bila jina alisema ...

safi sana....kitime vp hali ya gurumo?

Mzee Bob Hensen alisema ...

Mpenzi ya watu marehemu Dr. Remmy Ongala,baada ya kifo yake, atakumbushwa sisi daima, kwa sababu muziki yake inafika moyo!
Rotterdam, Holland.

Jay alisema ...

Kitime, ahsante sana kwa kujitolea muwanga na kutupasha habari za wasanii wetu bila kulipwa.