LAPF

LAPF
LAPF

Ijumaa, 17 Desemba 2010

Msiba mwingine katika jamii ya wanamuziki wakongwe

Abou Semhando Mungu akulaze pema peponi.
Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari. Abou ambaye kati bendi alizopigia ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.
Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo. Jambo la kusikisha pia ni kuwa Abou alikuwa moja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake.
Gari lililohusika katika ajali

Pikipiki ya Abou

Gari lililohusika katika  ajali hiyo

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

sad, sad

Baraka Mfunguo alisema ...

RIP -MUNGU AKUWEKE MAHALI PEMA PEPONI ABOU ALI SEMHANDO.