LAPF

LAPF
LAPF

Jumamosi, 18 Desemba 2010

Msiba wa Abou unaumiza sana

1. Leo ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba likizo
3. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.
Waliosimama..Remmy Ongala, Abuu Semhando,Kasaloo Kyanga, Fan Fan

3. Alikuwa mpiga drum wa Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka. 1981

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

RIP Abuu Semhando. Kifo cha Semhando ni pigo kubwa sana kwa fani ya muziki Tanzania. Hiyo picha Balozi inanikumbusha mbali sana. Waliochuchumaa kutoka kulia kama sikosei ni Skassy Kasambula, Hamza Kalala na ..... ah, huyo wa tatu sikumbuki. Msaada Balozi.

Bila jina alisema ...

Wamefuatana wote wawili, inasikitisha sana lakini ndio mipango ya Mungu. RIP Remmy na Abou.

J.Katanga

Jay alisema ...

Nakumbuka kikosi hiki pale Mwananyamala Komakoma, hii ilikuwa timu Kali kweli kipindi kile, nyimbo walizotoa ni pamoja na Alimasi, Usia, Onyo, Nalilia Mwana, Ndumila kuwili, na Tembea Ujionee.

Baba Diana hatuna Shaka kwani twafahamu Mungu yu nawe!

Bila jina alisema ...

Huyu wa tatu(Walio chuchumaa) ni Kulwa mpiga trumpet,enzi hizo alikuwa bado mdogo mdogo,baadae alijiunga na Vijana Jazz.
Abbu Omar,Tokyo,Japan.

Kisondella, A.A alisema ...

Katika historia mbali mbali za Marehemu Dr. Remmy nimekuwa nikisoma kuwa katika mazingira aliyozaliwa hakutakiwa kukata nywele, ndivyo tulivyozoea kumumona Remmy akiwa na rasta, hapa namuona Remmy akiwa na afro nzuri kabisa, inakuwaje?! Nachanganyikiwa!.

Abuu Semhando (R.I.P), namuheshimu sana katika upikaji wa drums, nafikiri ni mmoja ya wanamuziki hodari ambaye hatosaulika katika fani hiyo. Wasalimie Chipembele Said (Drums - Sikinde), Gabby Katanga (drums - Chuchu/Pamo/TOT),Moddy Terminator (Drums - Chuchu/Pamo/), n.k

Ulitoka mbali na Dr. Remmy sasa unamfuata,

Ningejisikia faraja iwapo Twanga na bendi nyingine zingemuenzi mwanamuziki huyo kama tulivyoshuhudia kwa mazishi ya Dr. Remmy

emu-three alisema ...

Inasikitisha sana, lakini ndio dunia, wametangulia sisi tupo nyuma yao!