LAPF

LAPF
LAPF

Alhamisi, 16 Desemba 2010

Remmy Ongala hatimae azikwa leo


 Dr Remmy hatimaye amelazwa kaburini, katika siku ambayo ilionyesha kuwa kweli Remmy alikuwa kipenzi cha watu. Siku ilianza kwa sanduku la mwili wa marehemu kuwasili katika uwanja wa Biafra Kinondoni B, saa nne kamili muda ambao ulipangwa. Gari jeusi la jeneza lilitanguliwa na pikipiki mbili za polisi.


 Baada ya gari hilo  kufika uwanja wa Biafra, ambapo tayari familia ya marehemu  ilikuwa imeshafika kukiweko na wanamuziki na vyombo vyao na pia wapenzi na ndugu na jamaa wengi, sanduku liliwekwa katika jukwaa maalumu chini ya tent jeupe. Bendi mbalimbali zilipiga muziki, zikiwemo za muziki wa enjili , bendi ya wasiojiweza, na kadhalika. Muungano wa Bendi za Enjili ulipiga wimbo ambao waliutunga na kuurekodi maalumu kumuaga Remmy.
 Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo  alikuweko na pia walikuweko wabunge wa Kinondoni na Ubungo, Mheshimiwa Iddi Azan na Mheshimiwa John Mnyika. Jaji John Mkwawa, wawakilishi wa BASATA, COSOTA, SHIWATA, wasanii wengi wakiwemo Mzee Jangala, Khadija Kopa, na wengine wengi

Kati ya vitu vilivyonitoa  machozi ni pale ulipopigwa wimbo wake aliyoutunga na kuuimba wakati akiwa Orchestra Makassy, ‘Siku ya Kufa..


 Baada ya Ibada na hotuba kutoka kwa Cosmas Chidumule kwa niaba ya wanamuziki na Mheshimiwa Dr Nchimbi, mamia ya watu walipita mbele ya mwili wa marehemu kumuaga. Jua lilikuwa kali sana lakini watu hawakujali.
 Kisha kwa msafara wa mapikipiki tena mwili ulihamia katika ukumbi wa Giriki Sinza baada ya kupitia kwa muda mfupi nyumbani kwa marehemu. Hapo ukumbini mamia ya watu tena waliweza kumwaga mwanamuziki wao mpendwa.
Hatimae saa kumi kama ilivyotamka ratiba mwili wa marehemu uliwasili katika makaburi ya Sinza na maneno yake katika wimbo Siku ya kufa, Binadamu nyama ya udongo yalitimia.

Hakuna maoni: