LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 2 Januari 2011

Msiba mwingine Mpiga Bass wa Sikinde Ngosha hatunae tena kafariki mchana huu

Marehemu John CharlesNgosha ni wa pili toka kulia katika waliochuchumaa, wa tatu ni  Marehemu Abou Semhando, picha ilipigwa mwishoni mwa mwezi wa sita wanamuziki wakongwe walipokutana na kula chakula cha mchana pamoja.

Marehemu John Ngosha

Msiba mwingine katika kundi la wanamuziki wa zamani. Mpiga Bez mashughuli John Ngosha wa DDC  Mlimani Park,Sikinde  hatunae tena Mungu amempenda zaidi. Taarifa zaidi zinafuata.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Poleni sana kaka zangu wa Sikinde
kwa kumpoteza ndugu Ngosha,ni pigo kubwa sana kwetu wanamuziki na watanzania wote.Kwa mara ya mwisho nilikutana nae pale ddc Kariakoo mwezi Feb.2010,hii ilikuwa katika kuwatembelea Sikinde,nakumbuka tuliweza hata kutaniana nae,maskini kumbe ilikuwa ni kuagana.Ngosha alikuwa "Ngouma Lokito"wetu huko Tanzania kwa upigaji wake mahiri wa bass.Tutamkumbuka milele.mungu ailaze roho yake pahali pema peponi.
Abbu Omar,Prof.Jnr.(Mwanamuziki,Japan)

Kisondella, A.A alisema ...

Inasikitisha lakini ndivyo ilivyo, Nasikitika sana kuona wapiga vyombo mashuhuri wanaondoka huku waliach apengo kubwa kwa waziba nafasi zao. Nashukuru Ngosha kwa kum-groom Tony Karama katika kupiga bass, natumaini Tony atazidisha ufundi zaidi, na kuongeza nidhamu katika kumuenzi Ngosha. Ngosha anawafuata wanamuziki wenzake ambao alipiga nao bebdi moja na ala moja (bass), Muhidini Kisukari, Suleman Mwanyiro