LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 3 Januari 2011

Mwanamuziki Mustafa Ngosha azikwa Mzee muhidin Gurumo ahudhuria mazishi

Juma Choka mpiga drum wa Sikinde alieongoza kwa utani wa jadi katika msiba na kudai chakula atakachopewa lazima kiwe na nyama, maana Wasukuma hufuga sana ng'ombe au la hata kula

Dua zikiendelea nyumbani kwenye msiba wa marehemu

Cosmas Chidumule ambaye ndiye aliyemleta Dar marehemu kwa kumchukua Mzinga Troupe ya Morogoro na kumuingiza Sikinde

Ally Jamwaka, na wa kati ni Malik Star ambaye wakiwa na marehemu walizunguka nchi nyingi kama wanamuziki wa Kanda Bongoman

Mchango wa papo kwa papo wa wanamuziki

Dede na Mafumu wakihamasisha mchango

Mwenye kofia ni Banza Stone akitoa mchango wake


Kikao cha dharura cha wanamuziki

John Ngosha mtoto wa marehemu nae ni mwanamuziki wa kundi la Rufita Connection

Mzee Muhidini

Group photo ya wanamuziki wakongwe

King Kiki na Mzee Muhidin
Msafara kuelekea Makaburini

Barabara zilifungwa kwa muda

Mzee Said Mabela mpiga solo wa Msondo

Abdallah Mgonahazelu mwimbaji Vijana Jazz

Choky na Babu yake

Huluka Uvuruge mpiga gitaa Msondo
Wanamuziki wengi wakiongozwa na Mzee Muhidin Gurumo wameshiriki katika mazishi ya mwanamuziki mwenzao aliyefariki jana baada ya kuugua. Mamia ya ndugu majirani na wapenzi wa muziki walishiriki katika mazishi hayo ambayo maandamano yake yaliweza kufunga barabara kwa muda, kuonyesha kupendwa kwa Ngosha na muziki wake kwa ujumla. Ngosha amelazwa katika makaburi ya Magomeni Ndugumbi

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Mkuu Kitime,utakapopata nafasi ya kukusanyika tena na wanamuziki wa Sikinde au wengine waliohudhuria msiba wa ndugu yetu Ngosha,wape salaam zangu za pole kutoka hapa Tokyo,najua watu wengi huko hawana tabia au hawatumii internett kabisa
kwa hiyo nifikishie salaam zangu kwa mdomo au njia yoyote uionayo ni bora kwa kufikisha ujumbe wangu.
Ingawa niko mbali na nyumbani lakini huwa nafuatilia sana habari za huko,za muziki na za nchi kwa ujumla.Kalale pema nddddugu yetu,mwanamuzi mashuhuri Tanzania
Mustafa Ngosha."Rspect"
Abbu Omar Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

SIMON KITURURU alisema ...

R.I P Mustapha Ngosha!

majaliwa alisema ...

Nimesikitishwa sana na kifo hiki kwangu ni pigo kubwa kwani mimi ni mpenzi mkubwa wa sikinde kwa miaka mingi na ngosha amekuwa kiungo mkubwa kwa bendi yetu hii,
Mwenye enzi mungu amrehemu!
Majaliwa Rubuye-Mpanda Rukwa