LAPF

LAPF
LAPF

Jumatano, 5 Januari 2011

Safari Trippers walikuwepo na bado wapo

Safari Trippers
Ni vigumu kupima raha ambayo Safari Trippers waliitoa na wanaendelea kuitoa katika ulimwengu wa muziki. Nyimbo zao bado zinapigwa na bendi chungu nzima mpaka leo hii. Unawajua walikuwa akina nani? Hiyo ni picha ya wanamuziki vijana hawa. Wadau tuanze kwa kuwataja wanamuziki hawa

Maoni 28 :

Jay alisema ...

Hapa namjuwa mmoja tu ambaye ni Marijani Rajab wa pili kulia kwa waliosimama.

Bila jina alisema ...

DAVID Gordon-Mussa [founder of the band]; and Msiba... the rest I don't recall...

Bila jina alisema ...

Hapo mimi namtambua Marijani tu aliyesimama wa pili kutoka kulia. Balozi, hii tumechemsha, tutajie hao wengine.

Sam Mnkande alisema ...

I also see Marijani and Patrick I believe

Bila jina alisema ...

Marijani wa pili kulia waliosimama, mbele yake in Christian Kazinduki, I presume.

Bila jina alisema ...

David Gordon (mwenye miwani), Ibuni Saleh (big question mark: wa kwanza kushoto waliochuchumaa???), "Becket" au Golden Samson (wa pili kushoto waliochuchumaa???; lakini another big question mark). John, huna budi ku-refresh kumbukumbu zetu. Mzee wa sasa, Kijana wa zamani.

Michuzi alisema ...

mie namkumbuka pia Ally Rajab (RIP) wa pili kulia nyuma, akifuatiwa na David Mussa, Christia Kazinduki na Dozza. JFK tumalizie basi. Enzi hizo picha mnapiga studio, raizoni, bugaluu na shati la kubana na bizbo. Acha!

Bila jina alisema ...

Upande wa kushoto chini mwenye saxaphone ni Mohamed Ibuni Saleh

amina alisema ...

Aliyeshika Trumpet is my dad Mohamed Ibuni Saleh yupo chini kushoto, now he plays piano as well.

amina alisema ...

Aliyeshoka Trumpet ni Mohamed Ibuni Saleh (baba yangu) he leaves at Kariakoo now, he plays piano as well.

Bila jina alisema ...

Namuona Marehemu Mahdi Tumbo aliyekaa na gitaa kama sijakosea..

Bila jina alisema ...

Huyo chini aliyeshika trumpet ni baba yangu Mohamed Ibun Saleh anakaa Kariakoo, ni architect, anapiga na piano and song writer.

Anapenda sana muziki and najua atafurahi kuona picha hii.

Bila jina alisema ...

Some apples fall far from the tree! Sasa Bin/t Saleh hapo trumpet liko wapi? Cheka!!!

Hawa makamanda walikuwa wote Five Stars Field Marshal Generals. Ukisikiliza Roza Nenda Shule, Sauti Yako Nyororo, Rafiki si Mtu Mwema, Hanifa, Matinda, Sokomoko Ndani ya Nyumba, Nyerere wa Kwetu, Mama Shani, Maria, Georgina, Heshima ya mtu Kufanya Kazi, Mkuki Moyoni, Salama, Urithi, Shani (Instrumental) na nyimbo zao nyingine lazima upagawe kinamna.

Makamanda walikuwa wanalikamua Rhumba kisawasawa. Katika blowing waliblow kwenye Roza Nenda Shule. Saxphone zililindima kwenye nyimbo hii mpaka wazimu. Halafu snare drum edge ilikong'otwa na Musiba. Wakuu, na Bass na Rhythm na Solo guitar yalibaluzwa. Halafu vocals na tungo yenyewe, aagh jamani nyie hapana! Halafu kuna kipande wanalimwaga sebene hapo lazima usepetuke (Neno Kusepetuka Wazaramo watanielewa) hata kama hutaki. Utasikia high-hat, shakers, rhythm, bass na vocals mwenyewe utasimama usepetuke kama unacheza Vanga! Aarrghh wazimu.

Utamu mwingine unakuja kwenye Usiwache Mbachao, Nasikia Maneo Maneno na Nani Mchokozi. Kwenye Nani Mchokozi na Nasikia Maneno Maneno Dosser haungurumi kwa nguvu lakini hiyo vocal unison tangu mwanzo mpaka mwisho halafu unison play ya Rhythm na Saxphones na Heavy Bass halafu kuna Solo fulani lenye vionjo unique/peculiar vya Hayati Madi Tumbo.

Mkuki Moyoni kuanzia Shairi la nyimbo: Vina na Mizani, Uimbaji, Solo na Rhythm Guitars, Bass, halafu Saxphones zilivyopulizwa kwa ustadi. Jamani nyie!? Yaani acha tu!

Utunzi wa Safari Trippers ulikuwa umekamilika kuanzia ghani(Melody), midundo(Rhythm), mwafaka (Harmony) hadi maudhui ya tungo yanayoshabihi maisha ya Mswahili yaliyovikwa ndani ya Kiswahili fasaha na rahisi yanayoeleweka kwa Mswahili na msemaji mwingine yeyote wa Kiswahili.

Good Things Don't Last Long! Sokomoko ilikuja kama Mzuka na ikaondoka kama Mzuka! Lakini bado inazuka na itaendelea kuzuka. Leo baada ya miaka takribani miaka 30 tangu ilipovunjika Safari Trippers bado Sokomoko linavuma.

Mdau, Sokomoko damu, Helsinki, Finland.

Bila jina alisema ...

wa pili kulia ni marijani rajabu anafuatiwa na Chriss Kazinduki na anaefuata David Gordon[Mussa]na anaefuata ni Ally.

Bila jina alisema ...

Sokomoko ilikuwa sio mchezo bwana nakumbuka sana pale princess ilikuwa hatari tulikuwa bado vibint,tunakaa nyumbani pale mtaa wa mbaruku basi kama linapigwa barazani kwetu loo tulikuwa tunaruka ukuta.

ELVAN STAMBULI alisema ...

Nmkumbuka sana Ali Rajabu wa pili kushoto waliosimama, David Musa mwenye miwani, alikuwa akija sana Temeke jirani na mzee Nyunyusa na Marijani wa pili kushoto. Hawa walipiga katika harusi ya mjomba wangu mzee Chitukuro wakati huo nasoma shule nilikuwa mdogoo lakini ninayekumbuka mambo, mjomba alimuoa mama mmoja mtoto wa Askofu Sepetu, sasa wapo Masasi. harusi ilikuwa Fododhani Hoteli sasa Mahakama ya Rufaa pale posta.
stambuli elvan, dar

Bila jina alisema ...

Wow! I remember dancing to Les Trippers / Safari Trippers music in the good old "boogie" days. Man-oh-man, those dudes could really play music, like there was no tomorrow! They sure did their thing! The "Shing-a-Ling", "Boogaloo" riffs were beyond electric! God bless them all... the living, and the departed. You'll all never be forgotten!

Chang'ombe Girl
Manhattan, NY

Eva alisema ...

Mi nikisikia wimbo mkuki moyoni naacha shughuli zote that i was doing, nafunga macho na kusikiliza utamu wa muziki uliopangwa ukapangika. Utamu hadi kisogoni! what more can I say?

Bila jina alisema ...

Je, wadau kuna mtu yeypte anamkumbuka Beckett (jina lake hasa Golden Samson) alikuwa Chang'ombe/ Temeke late 60's early 70's na aliwahi kpiga kwa muda mfupi Trippers? Is the guy still around? Eddy.

Bila jina alisema ...

mheshimiwa david gordon yupo kwake changombe amepata stroke anajikongoja mara ya mwisho nilmwona kama miaka mitatu iliyopita sijui hali yake sasa.

Perez alisema ...

"...Sauti yako nyororoo naipendaa unapoimba..,
unanikumbusha mbali sana..,
hebu we Kaka imbaa..,

We hapo uliye mbeelee..."

yaani! we acha tu

Bila jina alisema ...

Anon wa 6:16 AM, nilikutana na kaka yake David Gordon (nadhani December) akaniambia kuwa David yupo kwake lakini hatoki sana. Mdau uliyemuulizia Beckett hata mimi ningelipenda kujua kama Becket yupo around kwa sababu sijamuona miaka na miaka.

Bila jina alisema ...

The guys rocked!
SAFARI TRIPPERS oyeeeee!

FunGirl...
London, England, UK

Bila jina alisema ...

According to Capital FM Dar yule 'fastest drumer' Msiba Abdala anaishi Paris tangu Trippers ilipovunjika

Bila jina alisema ...

JAMANI SAFARI TRIPPERS ILIKUA KIBOKO HAKUNAGA, NAKUMBUKA ENZI HIZO BADO NIKO MDOGO ILIKUWA SIKU YA SIKUKUU YA IDDI, NIMEENDA KIDONGO CHEKUNDU NA MAMA YANGU WAKAMBO BASI TUMEFIKA TU MTOTO WAKE MDOGO AKAANZA KUMSUMBUA, IKABIDI MAMA ANATAKA KURUDI NYUMBANI NA MIMI NATAKA KUBAKI KWANI TRIPPERS INAPIGA PALE PRINCES, BASI NIKABAKI MAMA AKARUDI PEKE YAKE HOME, MIMI NIKAINGIA MAGOMANI HUKU NINA WASIWASI KWANI BABA ALIKUWA MKALI SANA NIKARUDI HOME SAA TANO USIKU, BASI WEEE SIWEZI KUSAHAU NILIPIGWA NA MZEE MPAKA BASI TENA,ILIKUA SAFI SANA ENZI ZILE SI MCHEZO.

Bila jina alisema ...

Rest in peace DAVID GORDON...

Kombo alisema ...

Katika maisha yangu kamwe sitamsahamu jabali la muziki Marijani Rajabu na bendi nzima ya safari tirppers. Kwa sasa sasa umri wangu ni miaka hamsini na nne lakini katika umri huu naweza kusema kwa upande wangu sijapata kuona ubora wa wanamuziki kama huu wa TRIPPERS hasa ukilinganisha na umri wao kwa wakati ule. Walikuwa ni vijana wadogo lakini mungu aliwajaalia uwezo mkubwa wa kuona mambo ya hekima na busara ambayo wao waliyafikisha kwa jamii kwa njia ya muziki.

Unawakumbaka akina Kiliongo, Ali Rajabu, Tabu tumbo, David Musa, kazinduki na wengine?

Marijani Rajabu ambae alikuwa akiwaongoza vijana hao, naweza kuzema ni mwanamuziki wa karne kwa Tanzania. Karibu nyimbo zote alizotunga ama kuimba zina ujumbe ambao hadi leo ukisikiliza bado maana na haja ya ujumbe huo ipo. Nyimbo kama Utamaduni, unakwenda wapi (mtoto mpotevu), Roza, sauti yako Nyororo, barua yako, mapinduzi, salama, mkuki moyoni, Geogina n.k

Nasema kwangu mimi wimbo “ndugu wa mtoto” umenigusa sana. Umegusa maisha yangu. Umegusa hali halisi ya maisha yangu. Ilifika wakati nikasema huyu Marijani na wenzake wa Trippers kama ingalikuwa naishi nao jirani basi ningesema wameniimba mimi. Huwa najiuliza waliwezaje kumuona mtoto huyu?.

Ah Mungu mlaze pema peoponi Marjani na wenzake waliotangulia.
Wape afya njema wana trippers walio hai

Nikimbuka nalia. Nawalilia Marijani na wenzake, Naikumbuka familia ya Marijani,
Kwangu naiona kama tu famila moja, Namkumbuka Mungu na uwezo wake,

MUNGU TUPE SUBIRA
AMINAWIMBO: NDUGU WA MTOTO

Enyi ndugu Enyi ndugu, Enyi ndugu wa mtoto Mbona hamuonekani, Siku hizi mko wapi nyieeeee?

Tangu mzee amekufa, Nyumbani mmeondoka, Na mtoto kumtupa, Sasa atamlea nani huyoooo

Mmeondoka mnajua, Mtoto bado mdogo Kwa kuwa roho zenu mbaya, Mnajifanya hamjali nyieeee

Wala hamkumbuki wema, Baba yake aliotenda
Wakati akiwa mzima, Mbona kawasaidia sana nyieeeee

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujua, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyiiiiii

Marijani
Isije ikawa kiguu na njiaaaaa, kwa mtoto nyumbani awasaide na shida zenu aibu

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujuaaaaa, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyiiii

Marijani
AAA bandugu nisikize kwanza. Muangalie mtoto bandugu

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujua, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyi

Yussauf H Kombo
+255 772 37 17 01
yhkombo@yahoo.com, yhkombo@hotmail.com

Kombo alisema ...

BENDI: SAFARI TRIPPERS
WIMBO: NDUGU WA MTOTO

Katika maisha yangu kamwe sitamsahamu jabali la muziki Marijani Rajabu na bendi nzima ya safari tirppers. Kwa sasa sasa umri wangu ni miaka hamsini na nne lakini katika umri huu naweza kusema kwa upande wangu sijapata kuona ubora wa wanamuziki kama huu wa TRIPPERS hasa ukilinganisha na umri wao kwa wakati ule. Walikuwa ni vijana wadogo lakini mungu aliwajaalia uwezo mkubwa wa kuona mambo ya hekima na busara ambayo wao waliyafikisha kwa jamii kwa njia ya muziki.

Unawakumbaka akina Kiliongo, Ali Rajabu, Tabu tumbo, David Musa, kazinduki na wengine?

Marijani Rajabu ambae alikuwa akiwaongoza vijana hao, naweza kuzema ni mwanamuziki wa karne kwa Tanzania. Karibu nyimbo zote alizotunga ama kuimba zina ujumbe ambao hadi leo ukisikiliza bado maana na haja ya ujumbe huo ipo. Nyimbo kama Utamaduni, unakwenda wapi (mtoto mpotevu), Roza, sauti yako Nyororo, barua yako, mapinduzi, salama, mkuki moyoni, Geogina n.k

Nasema kwangu mimi wimbo “ndugu wa mtoto” umenigusa sana. Umegusa maisha yangu. Umegusa hali halisi ya maisha yangu. Ilifika wakati nikasema huyu Marijani na wenzake wa Trippers kama ingalikuwa naishi nao jirani basi ningesema wameniimba mimi. Huwa najiuliza waliwezaje kumuona mtoto huyu?.

Ah Mungu mlaze pema peoponi Marjani na wenzake waliotangulia.
Wape afya njema wana trippers walio hai

Nikimbuka nalia. Nawalilia Marijani na wenzake,
Naikumbuka familia ya Marijani,
Kwangu naiona kama tu famila moja,
Namkumbuka Mungu na uwezo wake,

MUNGU TUPE SUBIRA
AMINAWIMBO: NDUGU WA MTOTOEnyi ndugu Enyi ndugu, Enyi ndugu wa mtoto
Mbona hamuonekani, Siku hizi mko wapi nyieeeee

Tangu mzee amekufa, Nyumbani mmeondoka
Na mtoto kumtupa, Sasa atamlea nani huyoooo

Mmeondoka mnajua, Mtoto bado mdogo
Kwa kuwa roho zenu mbaya, Mnajifanya hamjali nyieeee

Wala hamkumbuki wema, Baba yake aliotenda
Wakati akiwa mzima, Mbona kawasaidia sana nyieeeee

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujua, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyiiiiii

Marijani
Isije ikawa kiguu na njiaaaaa, kwa mtoto nyumbani awasaide na shida zenu aibu

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujuaaaaa, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyiiii

Marijani
AAA bandugu nisikize kwanza. Muangalie mtoto bandugu

KORASI - waitikiaji
Yangu ni mengi hamuwezi kujua, Huyo mtoto anakuwa atakuwa nanyi

Yussauf H Kombo
+255 772 37 17 01
yhkombo@yahoo.com, yhkombo@hotmail.com