LAPF

LAPF
LAPF

Jumamosi, 19 Februari 2011

Super Kamanyola ya Mwanza


Seseme ambaye ndiye mpiga Solo hapa akiwa amnapiga Bass

Benn Villa Anthony

Mukumbule Parash

Akiwa na Sax ni Roy Mukuna na kundi zima la Super Kamanyola

Beno na Parash

Anna Mwaole

Bonny Chande

John HamisiRoy Mukuna Kiongozi wa Bendi
Mwaka 2006,wanamauziki kadhaa wa zamani walijikusanya na kuanzisha bendi ambayo ilijulikana kama Tanza Muzika, bendi hii ilikuwa na wanamuziki kama akina Kasongo Mpinda Clayton, Issa Nundu, Mukumbule Parashi na wengine wengi wazuri. Pamoja na kuwa bendi nzuri walikosa vyombo na hivyo kuwa chini ya himaya ya jamaa walioweza kuwa na vyombo, ambao nao mwaka 2007 wakajitoa na hivyo kundi hilo kuvunjika. Wanamuziki wachache wakahamia Mwanza na kuungana na  kundi la Mwanza Carnival, hao walikuwa Roy Mukuna, Seseme Omary,Mukumbula Parashi,Issa Nundu, Bonny Chande . Miezi michache baada ya kuanza kwa kundi hili mfadhili wa kikundi akaanza kuugua na hivyo kundi hilo kusambaratika tena.. Wanamuziki wakaamua kurudi Dar Es Salaam na huko Ally Yahaya, ambaye ni mpiga trumpet nae akajiunga nao na wakajipa jina jipya Super Kamanyola. Na ni wakati huu wakaalikwa kwenye bonanza la Villa Park Mwanza, si muda mrefu baada ya hapo uongozi wa Mwanza Villa Park ukaingia katika makubaliano ya  kuifanya Super Kamanyola kuwa resident Band. May 2010 bendi ikahamia rasmi Mwanza. Kundi hili lina wanamuziki wafuatao.Roy Mukuna, Saxophonist na Kiongozi wa Bendi, Ally Yahaya Trumpetist Katibu wa bendi, Seseme Omary Solo guitar na uimbaji, Beno Villa Anthony mwimbaji na mpiga Keyboards, na pia mshauri wa bendi, Mukumbule Parashi muimbaji, Rashid Mwezigo mwimbaji, Anna Mwaole muimbaji, Bonny Chande Bass guitar, John Hamisi rhythm guitar, na Duncan Matembe Drums. Kwa kweli ni burudani kuisikiliza bendi hii ambayo ikiwa inapiga nyimbo za zamani za Maquis, OSS, Tancut Almasi, TP OK Jazz, African Fiesta, utadhani unazisikia bendi zenyewe.Maoni 3 :

Perez alisema ...

"...Ufitinaaa...
na upelelezi ni sumu ya mapeeenzi....,
..Ufitinaaaa, na upelelezi ni sumu ya mapeeenzi...

Mimi kupendwa na yeye,
nyinyi mwakerwa na nini eee,
Tumependana wenyewe bila nyinyi kujua,
Sasa mwajua mwaanza kuleta matataizooo.

...nyinyi mwakerwa na nini ee ee ee eeee..

Yeye kanipeeenda nami nampeeenda...

Mukumbule Lulembo Parash huyo mwanangu na sauti lake la kutetemeka.

We acha tu!

Bila jina alisema ...

Aliyeimba wimbo huu siyo Kasongo Mpinda??labda huyu Parash alishriki katika kuitikia lakini nakumbuka lead vocals zilitawaliwa na Kasongo Mpinda,hata mimi niliupenda sana wimbo huu,mkuu Kitime nisaidie namna ya kuupata,hata ni kama kwenye website,nionyeshe website hiyo ni ipi ili niupate wimbo huu,respect.
Abbu Omar,Prof.Jnr,Tokyo,Japan.

Bila jina alisema ...

Super Kamanyola band fanyeni hima mtuwekee clips za uhakika ktk youtube ili mzidi kupata sponsorship za makampuni ya vinywaji ya Tanzania kuongeza kipato.

Jiji la Mwanza ni kubwa na Tanzania ni kubwa.