LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 27 Machi 2011

Mzee Saidi Mabela anyakua tuzo ya Hall of Fame


Mzee Said Mabela, mpiga solo mahiri wa Msondo Ngoma, amepewa tuzo la Hall of Fame, heshima binafsi kwa kudumu bila kuhama katika bendi ya Msondo tangu alipojiunga na bendi hiyo 1973. Tuzo hiyo aliipata katika usiku wa Kilimanjaro music Awards uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jumamosi March 26, 2011 (picha kwa hisani ya www.michuzijr.blogspot.com)

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

Well deserved. He is one of the wakongwe wa muziki Tanzania.

Mzee wa Changamoto alisema ...

HATIMAYE........Niliandika August 18, 2009 (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/ni-lini-tutawaenzi-watu-hawa.html) kuhusu kuwaenzi hawa watu, na niliweka maandishi maalum kuhusu Said Mabera nikisema "Ni matawi haya ya serikali (kama CHAMUDATA na BASATA) ambayo yangestahili kusimamia thamani ya wanamuziki hawa kwa kuwatengenezea kumbukumbu maalum na hata tuzo za heshima kama HALL OF FAME kwa fani mbalimbali.
Kutofanya haya, ndiko kunakoweka DHARAU katika fani. Tunaona namna ambavyo watu wanathaminisha waimbaji wa sasa na WANAMUZIKI ambao wamefanya mengi ya maana kwa jamii na hakuna KIPIMO chochote cha kuwalinganisha. Leo hii waimbaji "chipukizi" wanawekwa kwenye kundi moja na watu kama Mzee Said Mabera ambaye licha ya heshima katika utunzi na utumiaji ala za muziki lakini amekuwa mfano wa kuigwa kwa kutohamahama bendi (yuko na Msondo kwa zaidi ya miaka 35), kutoropoka hovyo kwenye vyombo vya habari (kama wafanyavyo wengi sasa hivi katika kujitafutia majina) na pia kuheshimu maadili ya kazi. Wapo wengine wachache kama hawa. lakini hawana KINACHOWATHAMINISHA toka kwa walezi wao (Baraza la Sanaa ama Chama cha muziki wa Dansi). Kuna haja ya kuwaenzi kwa kuwaweka katika kumbukumbu na kuwapa TUZO ZA HESHIMA kulingana na kazi yao nzito." NAFURAHI KUWA MWAKA MMOJA NA NUSU BAADAE....WAMESIKILIZA

Bila jina alisema ...

Sahihisho. Said Mabera si miongoni mwa waanzilishi wa Msondo Ngoma ambayo ilianzishwa mwaka 1964. Mabera alijiunga na bendi hiyo mwaka 1973 na hajahama tangu wakati huo.

Bila jina alisema ...

Hapa naweza kusema bila kusita kuwa Mabera ndio Nguzo ya Msondo kwa takriban miaka 37 sasa. Kama Mabera naye angekuwa ni mtu wa kutangatanga sidhani kama Msondo ingekuwepo hadi leo hii. Mabera ameiwezesha bendi kuhimili mapigo mfululizo ya kuondokewa na wanamuziki mahiri kama Abel Balthazar, aliyeihama mwaka 1977, Muhidini Mwalimu (1978), Hassan Bichuka (1979), Shaaban Dede (alifukuzwa 1982 kabla ya kurejea 1987), Fresh Jumbe (1985), Kassim Mponda (1985) na Suleiman Mbwembwe (1987). Mabera anastahili tuzo aliyopata.