LAPF

LAPF
LAPF

Jumanne, 15 Machi 2011

Shaaban Dede ajiunga na Msondo kwa mara ya tatu

Shaaban Dede akipata chakula, wa pili Ally Jamwaka Mpiga Conga wa Mlimani Park na Shaaban Lendy Mpuliza Saxaphone maarufu
Shaaban Dede aliingia katika anga ya muziki wa Dar es Salaam kwa kupitia Msondo Ngoma , baada ya hapo alikwenda Bima Lee, akapitia Mlimani Park, akarudi Msondo, akaenda Mlimani tena karudi Msondo tena, Je, safari imekwisha? ngoja tutamsikiliza Dede mwenyewe kupitia blog hii hii.

Maoni 13 :

Bila jina alisema ...

Hapa naona mkuu Dede umetutosa sisi wapenzi wa Sikinde,wewe ndiye uliyekuwa nahodha wa meli yetu,MV Mapenzi, meli ya wapendanao,sasa naona umejitosa baharini !!! angalia usije ukamezwa na papa na nyangumi wenye uchu !!!
mpenzi wa Sikinde,Kariakoo,Dar

Kisondella, A.A alisema ...

Kimsingi nimesitushwa sana na habari ya Dede kurudi msondo,kinachonifanya nisituke ni kwamba Dede ni an damu ya Sikinde japokuwa kabla ya kuja Sikinde alitokea Msondo

Pili ni kwamba Dede alikuwa na ugonjwa wa kuhama bendi, naasikitika kuwa ugonjwa huo umerudi tena (kiasi ambacho nashawishika kumshauri aende Loliondo kwa "Babu" akapate kikombe ili akili irudi vizuri

Aidha sijui nini kimetokea ndani ya Sikinde mpaka ameamua kuchukua uamuzi huo.

Bwana Kitime mineshindwa kusubiri Dede mwenyewe atuleleze nini kimejiri, lakini nikiwa mdau mkubwa wa sikinde nimeaona nianzie hapa

Kisondella - Mafinga (Iringa)

Bila jina alisema ...

Mkuu Dede hapa umetutosa,kwenda Ottu !!Wewe ndiye nahodha wetu tuliyekutegemea kuongoza meli yetu ya wapendanao,MV,Mapenzi,sasa dhoruba imetokea na umeamua kujitosa baharini !!jamani !!agalia sana huko baharini kuna papa na nyangumi wenye uchu tena wale wa hatari,wasije wakakumeza masikini !!!mkuu Kitime mpe salaam hizi Dede,tunaamini zitamfikia.
mpenzi wa Sikinde "damu"Kariakoo,Dar.

GESHNA alisema ...

Haa! tena mpambano ndiyo kesho tu kwa nini tena Dede watufanyia hivyo wana Nginde. Lakini yote sawa tutakaza moyo na kukumiss sana katika jukwaa la Ngoma ya Ukae. Pia wadau nimepata taarifa kuwa Benno Vila anampango wa kurejea Sikinde. mwenye taarifa rasmi wakuu.

emu-three alisema ...

Hapa shabani dede, huku muhidini Ngurumo, nani tena,Bichuka...ilikuwa kazi!

`Shabani dede oooh, siwezi, ...'

Perez alisema ...

"...bomu la uzima wangu limepasuka hadharani..
nilipoingia ndaani, nisimkute mwana,
Tausi wangu miimi, katooweka..."

wee acha tu

Bila jina alisema ...

Mimi Sikinde damu na nimesikitika sana Dede kuondoka. Lakini pia nimefurahi.
Nimesikitika kwanini? Kwa sababu Dede ni mmoja wa waimbaji ambao wameibeba sana Sikinde kipindi cha karibu miaka 15 hivi. Na kuna wakti walibaki waimbaji 3 tu, yeye marehemu Mwinyikondo na marehemu Lubua. Dede aliendelea kuwapo Sikinde na kuisaidia, hivyo alikuwa Sikinde damu japo alipata kupiga msondo.
Lakini, nimefurahi kujua kwamba kumbe huu muziki wa Dansi bado unaheshimika tena sana tu. Kuondoka kwa Dede, tumejionea media coverage kutoka karibu magazeti yote, vituo vya television, radio na kadhalika, vikiliongelea jambo hili kwa mapan na vingine vikifanya mahojiano ya moja kwa moja na Dede. Hii ni nzuri, kwa wanamuziki hawa kujua kwamba dansi bado ina wapenzi na watu wanaifuatilia ni wao tu kukaza buti. Maana kipindi cha nyuma ungeasikia kwamba vyombo vya habari vinaandika sana Bongo gfleva na kutusahau. Kumbe si hivyo.
Pia kuna manufaa ya mabadiliko ya namna hii kwa bendi zote mbili. Leo Jumbe karudi Sikinde,pengine kama Dede asingeondoka asingefikiria kurejea.
Benno Villa, yupo Mwanza na Super Kamanyola, mtazamo wangu, huyu ndiye angekuwa mwafaka zaidi pale Sikinde. BENNO NI sIKINDE DAMU NA HATA UTUNZI NA MAIMBIO YAKE KWENYE BENDI ZINGINE HAUPENDEZI KAMA AKIWA SIKINDE. Huyu ndiye Sikinde zaidi hata kuliko Dede,, wangeweza kumrudisha huyu ingekuwa bora sana kwao.
Tatizo la Sikinde ni pale wale wapenzi wao wanaojiita Sikinde family kutokuwa na msaada wa maana kwa Bendi inapotaka kujiimarisha. Wengi wako kwa kujinufaisha wao tu, tofauti na maseneta wa Msondo kama akina Kagusa, Rage,nk. Wako tayari hawa kutoa pesa ya kumnasa mwanamuziki wakimuhitaji pale. Lakini Sikinde family, nauli tu ya Benno toka Mwanza ni tatizo.
Kwa ujumla, mabadiliko haya japo yanauma, yana manufaa kwa muziki wa Tanzania ingawa ukweli unabaki pale pale kwamba msondo ndiyo wamelamba Bingo hapa kwa kumnasa DEDE.

Bila jina alisema ...

Dede kaondoka Sikinde, sawa!!! lakini tusihuzunike saana kwani bado tunaye stereo Bitchuka, ambaye ni mkali saaana kupita Dede, hebu sikiliza vitu kama Jerry,hadija,fikirini,tufurahi na wana sikinde,talaka ya hasira,mnanionyesha njia ya kwetu,duniani kuna mambo.,nk ni nyingi mno, ambapo Dede alitoka na kibao..Fatuma... ni nyimbo nzuri mno!!! classic.. lakini hamfikii Bitchuka kabisaaa!! kwa hiyo pengo si kubwa kiasi hicho,ingawa lipo.

SENETA WA MSONDO alisema ...

Pole jirani,usisikitike sana tulimtaliki kwa taraka rejea,leo amerudi nyumbani,karibu ndugu yangu DEDE,msondo ni nyumbani kwako ondoa shaka tunakukaribisha sooote kariiibu,karibu ndugu yetu.

Naona kwa jirani kuna msiba,pole jirani ndio ukubwa huo.

Bila jina alisema ...

Hakuna taabu jirani,kama unakumbuka vuri, miaka ya nyuma kundi la watu walihama kwa mpigo kutoka sikinde,lakini wanaume walijipanga na kutoa vitu vya nguvu!!!....na sio mara moja,kwa hiyo kuondokewa na mwanamuziki mmoja hakuna haja ya kuweka matanga!!....sitaki kuwa negative kuhusu Dede, ndio ni mwimbaji mzuri,lakini kaugonjwa chake cha kuhamahama kimemrudia,na unajua mwaka hamalizi hapo,au utakataa?

Bila jina alisema ...

Jambo moja ambalo washabiki wa sikinde na msondo inbidi tulikubali ni kwamba, Dede kaacha pengo sikinde, na ataacha pigo msondo.

Bila jina alisema ...

Ningependa hata Bichuka arudi msondo tena,Bichuka kaka tafadhali rudi nyumbani

Bila jina alisema ...

Watani......sasa naona mmeishiwa!!!