LAPF

LAPF
LAPF

Ijumaa, 27 Mei 2011

Bendi ya akina mama- Women Jazz

Ni mara chache kukuta bendi ya akina mama watupu, katika kumbukumbu zangu hii imetokea mara 4 hapa Tanzania. Mara ya kwanza ni bendi hiyo hapa pichani iliyochukua umaarufu sana wakati wake. Niko mbioni kukutanishwa na mmoja wa washiriki wa bendi hiyo ambaye naambiwa anaishi maeneo ya Mchikichini pale Ilala najua tutapata mengi toka kwake. Katika miaka ya 80, Baraza la Sanaa la Taifa lilihamasisha akina mama wanamuziki kuanzisha chama chao ambapo mwenyekiti wao alikuwa Marehemu Asia Darwesh, Chama hicho kiliitwa TAWOMA, Tanzania Women Musicians Association kilitengeza pia bendi ya akina mama ambayo haikudumu sana. Rulu Arts pia ilifanya jaribio kama hilo la kukutanisha akina mama ambapo waliweza kufanya show moja Russian Culture miaka hiyo ya 80. Katika kipindi cha karibuni, mdau mmoja tena aliweza kuanzisha bendi ya akina mama ambapo alifuata mambinti kutoka Congo, wakashirikiana na waakina dada wachache kutoka Tanzania, kundi hilo nalo halikudumu mda mrefu likafa. Women Jazz ilikuweko hewani katika miaka ya sitini, ilipokufa ndipo vyombo vyake vilitumika katika kuanzisha Vijana Jazz. Kuna wimbo mmoja ambao hupigwa kila Xmass, ukiimba  ihappy Krismass iyooo iyoo na kisha kuanza kutaja herufi za alfabeti ndio mmoja ya nyimbo za bendi hii

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Bro, (1) Nilipokuwa mdogo (miaka 5 mpaka 8) nakumbuka nilikuwa nasikia sana nyimbo za Frank na dada zake redioni. Nimewahi kusoma habari za Frank (Humpledink???) katika magazeti mbalimbali, lakini sijawahi kuona habari zozote kuhusu dada zake. Je, kuna mtu yoyote ana data zao? (2) Kama sikosei niliwahi kuona mahali fulani picha ya binti wa marehemu Mbaraka Mwinshehe akiimb. Je una data yoyote kuhusu maendeleo yake katika fani ya muziki? Ahsante sana.