LAPF

LAPF
LAPF

Jumanne, 28 Juni 2011

Mazoezi ya wanamuziki wakongwe yafikia patamuManeno Uvuruge


Matei Joseph

Kasongo Mpinda

King Kiki


Mtangazaji wa miaka mingi Abdallah Majura alitembelea kambi
Hali katika kambi ya wanamuziki wakongwe ni ya furaha na vicheko muda wote, utani wa hawa wanamuziki wakongwe unafanya mazoezi yaonekane yanachukua muda mfupi kila siku. Mazoezi haya ambayo hufanyika Jumatatu hadi Jumatano kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ni yenye mafunzo na utamu mwingi. Vibao vingi vya zamani vinapikwa upya na vibao vipya pia vimetungwa tayari kwa kuingia studio. Wageni ni wengi na huwa furaha kuu wakati watu ambao hawajaonana zaidi ya miaka 30 kuonana tena na kuchekana kwa wingi wa mvi au ukubwa wa kitambi.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

saante sana Meya kwa kutujuza yanayoendelea huko nyumbani ktk tasnia hii ya muziki. Nimesikitishwa pia kwa kutokuwaona baadhi ya wanamuziki wakongwe ambao mwaka jana walishiriki.
1. Said mabela wa msondo ngoma music band( Aibu kwako kwa kutokuwepo ktk kundi hili kipindi hiki.
Shaaban Dedewa Msondo.( Nilitegemea unazeeka vizuri kwa kuweza kuwa na fursa ya kujumuika na wenzio lakini wapi? kumbe bado ni KAMCHAPE TUU!
2.Hassan rehani bitchuka wa DDC mlimani pia hata wewe ni waajabu maana unaendeleza visa visivyo kuwa na maana.

Mzee shem karenga Tabora jazz .( na wewe pia huna hekima maaana umeweka maslahi mbele bila kujali utu. Nilidhani tunu yako ya kuimba na kupiga gitaa ungeliitumia kipindi hiki cha miaka 50 ya uhuru lakini kumbe ndio wale waleeeee? pole mzee mwenzangu kwa yote yanayo kukuta. Ndio maana wakongo wanatesa na tungo zako.
5. Kalamazoo nyembo,Hendry Mkanyia , Bindo bakari,Joseph mzeru Mohamed Mgoro na wengine woote ambao sijawakumbuka na hamkutaka kushitiki hapa AIBU KWENU MAANA MUZIKI WENU MNAENDA NAO KABURINI.
Meya kitime naomba uitundike hii kama ilivyooo usipunguze neno.
Ni mimi
Hasaan Mpiluka.
Mzee wa zamani ninaepiga box ughaibuni