LAPF

LAPF
LAPF

Jumanne, 14 Juni 2011

New Star Jazz Band ya Tanga

Waliosimama -Mwanyiro Suleiman(Computer) na Hassan Ngoma, aliyechuchumaa Mohamed 'Moddy' Mrisho, mwaka 1972
Tanga kulikuwa na bendi nyingi na kulikuweko na bendi kadhaa zilizoweza kupata umaarufu wa kitaifa na kimataifa. Jamhuri Jazz Band, Atomic Jazz Band, Amboni Jazz Band ni baadhi ya bendi ambazo hukumbukwa sana lakini pia kulikuweko na bendi nyingine ambayo haikudumu muda mrefu japo ilipata kurekodi nayo iliitwa New Star Jazz Band. Pichani wapigaji wa bendi hiyo katika mwaka 1972. Marehemu Suleiman Mwanyiro hukumbukwa sana kwa bezi lake na mbwembwe alizokuwa akizifanya wakati wa kupiga, hapa anaonekana akiwa na suruali zilizokuwa na lisani ya aina yake, staili hii ya ushonaji iliigwa kutoka kwa mwanamuziki James Brown. Maelezo ni kuwa bendi ilikwenda Nairobi kushonewa suruali hizo. Aliye pembeni ya Manyiro ni Hassan Ngoma huyu nyimbo ambazo alipiga Atomic Jazz kabla ya kuingia kwa John Kijiko zinapigwa na kuliwaza mpaka leo, kati ya hizo labda nitaje mbili, wimbo ule wenye maneno, Tanzania yetu ndio nchi yenye furaha , kote ulimwenguni watu wote watambua, Tanzania nia yetu ndiyo nchi ya kusifiwa. Pamoja na ule wimbo wa mapenzi Afidha wangu, ni kazi ya upigaji solo wa huyu bwana. Aliye chuchumaa bado anapiga muziki mpaka leo ni Mohamed Mrisho aliye katika kundi la Kilimanjaro Band, gitaa lake linajulikana sana kwenye nyimbo zote za Njenje, na hasa solo katika wimbo wa Kinyaunyau, Boko na kadhalika. Kumbukumbu safi sana hii.

Hakuna maoni: