LAPF

LAPF
LAPF

Jumanne, 14 Juni 2011

Ugeni wa watangazaji na mafundi mitambo wakongwe

James Mhilu fundi mitambo


Mazoezi ya wanamuziki wakongwe leo yalisimama kwa muda baada kundi la wakongwe watangazaji na mafundi mitambo wa RTD kuwasili katika kambi hiyo. Wakiongozwa na John Ndumbalo (Fundi Mitambo), walikuweko James Muhilu, Fundi mitambo ambaye amerekodi mamia ya nyimbo zinazotamba mpaka leo katika anga za muziki wa radio na 'live'. Maulid Ngongolo (fundi mitambo), watangazaji waliokuwa na majina enzi hizo nao walikuweko, kama vileSuleiman Kumchaya, Mohamed Ngayonga, Hamis makumbi walikuja kuwatakia mkono wa heri wanamuziki hawa ilikuwa ni uwanja wa stori nyingi za vituko vya studio enzi hizo

John Ndumbalo fundi mitambo

John Ndumbalo na Maulid Ngongolo

James Mhilu na Suleiman Kumchaya

Maulid Ngongolo na Hamis Mkumbi


Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Nimefurahi kumuona Suleiman Kumchaya. Niliondoka Dar mwaka 1991. Kama sikosei, mara ya mwisho nilonana na kuongea naye 1989 Uwanja wa Taifa Dar.