LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 3 Julai 2011

Sauti tamu ya Mzee Salum Zahoro

Mzee Salum Zahoro ana umri wa miaka 75,lakini mpaka leo yupo jukwaani akiendelea si tu kupiga gitaa lakini pia kuimba. Na sauti ya Mzee Zahoro bado ni ilelile tamu ambayo ilikuwa ikisikika katika nyimbo zake maarufu wakati huo akiwa Kiko Kids. Nyimbo kama Sili sishibi silali, Wamtetea nini, Na kakumpa na kadhalika hapa ni video yake ya wiki hii

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Nakumbuka enzi za utoto kule Tabora
tulikuwa tunaziona bendi kama Tabora Jazz na Kiko Kids zikitumbuiza mara nyingi mchana katika harusi na sherehe mbali mbali,Namkumbuka sana mzee huyu mzee Zahoro na nyimbo zake kama maua eeh maua mapenzi yaua,nashangaa Kiko,Nakakumpa kasiki nk.miziki hii nakumbuka hata mama zetu waliicheza enzi za ujana wao na wanamfahamu sana huyu gwiji wa muziki mzee Zahoro.Ni jambo la kushukuru sana mzee wetu hadi umri huu (75)bado anawasha moto katika majukwaa ukilinganisha maisha ya sasa ya wanamuziki na watu kwa ujumla ni mafupi sana.Big up mzee Zahoro.Pia asante sana mkuu Kitime kwa juhudi zako za kutulatea habari za muziki wa huko nyumbani.
Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

SIMON KITURURU alisema ...

POA sana!

Perez alisema ...

"..Ohooo ohoo hoho mwachieni huyo,
yaelekea hana kosaa....,
burebure mwafwata fwataa ni kosa gani alilolitendaa...

yaelekea hana kosaaa,
burebure mwamfwata fwataa, ni kosa gani alilolitenda.

....mwamtetea bure, si mtu mwema huyoo...


We acaha tu!