LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 22 Agosti 2011

Chakula kwa jirani ya Tabora Jazz Band

Nimekumbuka mashahiri ya wimbo Chakula kwa jirani ya Tabora Jazz wakiwa na mtindo wao Segere Matata. Namkumbuka Rafiki yangu Wallace Mkello aliyeupenda sana wimbo huu


Visa alivyotenda Wallace mama
Sintovisahau, maishani mwangu,
Alinidanganya nihame kwetu, kisha anipe tabu mimi,
Halali nyumbani Wallace sijui yu wapi.
Chorus
Chakula nakula kwa jirani jama
Mafuta ya taa kwa jirani jama
Mwishowe jirani wamechoka jama
Kulala na lala peke yangu jama
Tabora Jazz Band 1969/70
Wallace kanifukuza nende kwetu
Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Mkuu kitime kwenye picha hii ya Tabora Jazz,huyo aliyesimaa wa kwanza kulia(jacket ya track) ni mjomba wetu soloist wa kwanza kabisa kabla ya Shem Karenga Athmani Tembo(Baba Nyota)R.I.P,aliacha miziki akaingia kazi ya railway akafanya Shinyanga,Moshi,na kurudi Tabora alifariki muda mfupi tu baada ya kustaafu Railway,pia alipoacha miziki akawa mswalihina mtu wa swala tano,atakumbukwa sana kwa kuwa nae alikuwa guitarist mzuri sana.R.I.P uncle AthmaniTembo.
Abbu Omar,prof.Jnr.(Mwanamuziki)Tokyo,Japan .