LAPF

LAPF
LAPF

Jumamosi, 20 Agosti 2011

Muziki wa salamu za wagonjwa


Kwa wale waliokuwa wapenzi wa RTD watakumbuka kipindi kilichokuwa Jumapili asubuhi ambapo RTD ilitembelea hospitali mbalimbali na kuwawezesha wagonjwa watume salamu. kipindi kiliitwa 'Salamu za wagonjwa'. Wimbo ulioashiria kuanza na kuisha kwa kipindi hicho ulipigwa na mwanamuziki Mzee Kungubaya nimebahatika kupata tena picha yake huyu ndiye Kungubaya. Angalia hiyo stika kwenye gitaa mnakumbuka CO CABS?

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

mzee kungubaya yupo kibaha maili moja kwa sasa ni jirani yangu,mara nyingi humuona akikata mitaa na gitaa lake kwenye ma bar na ukimpa chochote anakupigia muziki,

John Mwaipopo alisema ...

du! hapa pa kupiga gitaa bar ndipo alipofikia ilhali RTD wameutumia wimbo wake kwa miaka mingi sana mpaka hivi karibuni