LAPF

LAPF
LAPF

Jumatano, 24 Agosti 2011

Unawakumbuka Orchestra Fauvette

Wapili toka kulia waliosimama ni marehemu Ndala Kasheba.
Hii ni bendi iliyokuja Tanzania na kutingisha anga la Afrika Mashariki na Kati. Kati ya wanamuziki waliokuwemo katika kundi hili ambao waliendelea kubaki nchi hata baada ya kufa kwa kundi hili ni King Kiki, marehemu Ndala Kasheba, marehemu Baziano. Wangapi unawakumbuka katika picha hii?

Maoni 1 :

Baraka Mfunguo alisema ...

Ingawa wakati wakiwa wanapiga muziki wao nilikuwa bado sijazaliwa, nilijaribu kufuatilia na kuweza kujua kidogo hawa jamaa walikuwa wakipiga muziki wao maeneo ya Kinondoni miaka hiyo. Na katika vibao vyao kuna kibao al-maarufu kama "Fransisca" na "Voyage Emonani". Binafsi nilimsikia Anko J. Nyaisanga akielezea historia yao katika kipindi cha "hizi nazo"