LAPF

LAPF
LAPF

Jumamosi, 3 Septemba 2011

Frank Humplick na dada zake


Mzee Frank Humplick Mtanzania, ndiye mtunzi wa nyimbo kama Kolokolola, Simba wa Bara, Tufurahi kwani leo harusi, (wimbo uliorekodiwa baadae na Afro70 na pia Mombasa Roots) na nyimbo nyingi sana ambazo bado zinapigwa na bendi nyingi hapa Afrika ya Mashariki. Mzee Humplick wakati wa mkoloni aliwahi kutunga wimbo uliyokuja kupigwa marufuku na santuri za wimbo huu kusakwa nyumba hadi nyumba ili kusibakie hata nakala ya wimbo huo? Maneno ya wimbo huo yalisema hivi:
Uganda nayo iende
Frank Humplick
Tanganyika ikichangaruka, Kenya na Nyasa zitaumana
Nasikia fununu wanavyoichanachana China, Kitisho!
I am a democrat, I don't want communism, English, Yes, No I don't know, Kizungu sikijui
Wanyika msishindane na Watanganyika 

Wimbo huo ukaanza kutumika kabla ya mikutano ya Mwalimu Nyerere na kuanza kuwa maarufu kama wimbo wa kudai uhuru, wakoloni haraka sana wakaona wimbo huu utaweza kusababisha vurugu kama ambazo zilikuwa zinaendelea Kenya chini ya Maumau. Serikali ikaupiga marufuku na kuanza kuusaka nyumba hadi nyumba
Kati ya mwanamuziki Mtanzania ambae historia haijamtendewa haki kutokana na kutothaminiwa kwa kazi zake ni marehemu Mzee Frank Humplick. Mzee Humplick  ameishi kwa miaka mingi ya mwisho wa maisha yake Lushoto. Mzee huyu akiwa na dada zake wawili walitikisa anga za muziki wa Afrika ya Mashariki, na bado wanaendelea kufanya hivyo japo hawatambuliwi kabisa. Kundi lao lililoitwa Frank na dada zake waliuletea ulimwengu nyimbo nyingi ambazo mbaya zaidi mara nyingi nyimbo hizo zimekuwa zikitambulishwa kama nyimbo za mwanamuziki mwingine kutoka Kenya marehemu Fundi Konde.

Hakuna maoni: