LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 5 Septemba 2011

Frank Humplick, ujumbe toka kwa mwanae

Kwa furaha ningependa kuweka ujumbe huu toka kwa mwanae Frank Humprick- John, kwanza kabisa nikupe shukrani kwa kuutambua mchango wa Marehemu Mzee Frank Joseph Humplick katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika. Kama mwanamuziki unatambua effort na creativity inayohitajika kutunga na kutoa wimbo. Baada ya kusema hayo ningependa kusema kwamba ni kweli Marehemu Mzee Frank Humplick alitunga nyimbo nyingi sana wakati akiwa 'active' kama mwanamuziki. Ni kweli pia kwamba baadhi ya nyimbo zake zimewapatia watu wengine (wakiwemo the Mushrooms Band kutoka Kenya) umaarufu pamoja na fedha hususan wakati ambapo nyimbo zinazojulikana kama 'zilipendwa' zilianza kuwa adimu na hivyo kusakwa sana. Lakini just to put the record straight, nyimbo 2 ambazo umezimetaja yaani, Simba wa Bara na Kola kolola siye yeye aliyezitunga. Hizo ni nyimbo za Marehemu Fundi Konde kama sikosei. Ila wimbo wa Tufurahi kwani leo harusi ni utunzi wake na watu wengi mpaka leo wanaamini kwamba wimbo huu ulitungwa na Bendi ya Afro 70 wakati si kweli. Nilitaka tu kuchangia hilo na Hongera kwa kutupa 'updates' za hapa na pale katika facebook. I enjoy reading your posts. BJ Humplick (mtoto wa Marehemu Frank Joseph Humplick)  
Shukrani sana BJ, Ni wazi kuna haja ya kukusanya na kuweka wazi list ya nyimbo za Frank na dada zake. Nitahakikisha nakuja na list iliyosahihi katika blog hii mapema iwezekanavyo. Bottom of Form

Maoni 1 :

Kambogo alisema ...

Shukran sana! Nakumbuka tulianza process ya kutafuta hati miliki wakati bado baba yangu yu hai lakini kutokana na sababu moja au nyingine hilo halikuwezekana. Si neno. Na mimi pia nitajaribu kuorodhesha nyimbo zao ninazozikumbuka. Just so you know, Marehemu Baba alikuwa anatumbuiza zaidi kwenye harusi na sherehe binafsi mbalimbali na mara nyingine hata kuombwa na watu aidha marafiki au washikaji tu, kutunga specific songs kwa ajili ya kufikisha ujumbe mahsusi - wa mapenzi au ujumbe mwingineo wowote.