LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 3 Oktoba 2011

Hebu pata vionjo vya MR2.....enzi hizoooooo

Mwaka 1995, nikiwa najaribu kusambaza kazi za wanamuziki wa Tanzania kupitia kajimradi kadogo, mwanamuziki Innocent Nganyagwa alinijia na kunihadithia kuhusu mwanamuziki mpya wa Rap ambaye alikuwa tofauti na wasanii wenzie, kimawazo na hata jinsi ya sanaa yake ilivyo, na ndipo nikakutana na kusikia kazi ya  MR2. Muziki wake ulinifurahisha kwa sababu mbili ya kwanza alikuwa akitumia Kiswahili kilichoeleweka tofauti na wasanii wengi wa Rap wa wakati huo ambao walighani Kiswahili utadhani wameshuka leo toka Marikani, pili alikuwa na ujumbe mzito, ambao hata leo miaka  zaidi ya 15 toka ulipotolewa bado una maana kwa jamii ya Tanzania. Sishangai kuwa yeye sasa ni Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi. Lazima nijisifu kuwa sikukosea kuanza kusambaza kazi yake ya kwanza album ya NI MIMI. Angalia video hii kwa makini utakuta mengi aliyosema atatimiza alitimiza.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Sugu ni mtu wa kipekee sana na mfano kwa vijana wa kibongo..wasanii mpeni suport anauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye game ya music bongo