LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 3 Oktoba 2011

Maoni ya mdau

The Legendary Safari Trippers, Marijani wa pili kulia kati ya waliosimama, wa kwanza ni Uvuruge mtunzi wa wimbo GeorginaNyumbani tulikuwa na video cassette VHS aliyorekodiwa Marehemu Doza(Marijan Rajabu) na Orchestra Dar International kwenye show yao moja kule Buguruni Casanova Bar ( Kama sikosei) kwa Mwalimu Msuya. Ngoja nitawauliza waungwana nijue iko wapi.

Marehemu Doza si tu alikuwa muimbaji, mtunzi na mpiga guitar bali pia alikuwa anajua kuusoma muziki. Nadhani nadharia ya muziki alijifunza shuleni Olympio na Tambaza kwa sababu wakati ule muziki ulikuwa bado unafundishwa shuleni. Muziki lilikuwa somo linalofundishwa shule ya Tambaza hadi miaka ya '90 sijui kwa sasa.

Nikisikiliza tungo za Safari Trippers huwa nasikia muziki uliotungungwa kitaalam haswa kuanzia kwenye ghani/melody, midundo/rhythm, vikolombwezo/harmon hadi tenzi/lyrics. Safari Trippers iliundwa na na baaadhi ya wanamuziki waliokuwa "wataalam wa muziki" wakiwemo David Mussa, Mohamed Ibun, Musiba, Marehemu Doza na Marehemu Cris kazinduki. Nakumbuka Marehemu Cris alikuwa anafanyakazi Wizara ya Elimu na alikuwa wakati mwingine anajam na Mzee Kibira (Baba yao kina Onesmo Kibira) wakipiga muziki kwenye sherehe mbali mbali pale Wizarani. Mzee Kibira alikuwa anapiga Trombone. Naomba mnisahihishe kama nimekosea.

Kwa kumalizia: Moja ya Disadvantage ya kukosa televisheni Tanzania ni kukosa hifadhi ya mambo mengi katika mfumo wa filamu.

Mkuu, tafadhali wasiliana na Televisheni Zanzibar uone kama kuna uwezekano wa kupata clips za muziki. Nakumbuka kuna ile show ya Marquis du Zaire waliyokuwa wanaionyesha katika sherehe za kuzaliwa CCM mwaka 1977. Pia unaweza kuwasiliana na Audio-Visual Institute Kijitonyama walikuwa wana materials za muziki kibao. Chuo cha Sanaa Bagamoyo walikuwa wanarekodi sana matukio wakati wa Tamasha nina hakika kutakuwa na clips nyingi tu za bendi mbali mbali zilizokuwa zinatumbuiza katika ufunguzi na maonyesho mengine wakati wa Tamasha. Mtu mwingine ambaye anaweza kuwa na materials ni Mohamed Kissoky na ni Prof. Martin Mhando nina hakika haya majungu kuu hayakosi ukoko.

Nakutakia kila la heri na mafanikio katika jitihada zako.

Mdau Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.

Maoni 7 :

Perez alisema ...

"...Sauti yako nyororoo naipenda unapoimba,
inanikumbusha mbali saana,
Hebu we Kaka imbaaa....

We hapo uliye mbeeleee..."

Yaani, we acah tu.

Bila jina alisema ...

Ahsante sana...all i can say is "those were the (good old) days my friend we thought would never end" na pia "no regrets" na kumshukuru Muumba wetu kwa kutupa ujana enzi hizo katika Bandari ya Salama.

Bila jina alisema ...

mdau aru sure mtunzi wa nyimbo Georgina n Mvuruge?

JFK alisema ...

Ndio Georgina ilitungwa na marehemu Jumanne Uvuruge, japo kutokana na kuimbwa na Marijani aliyekuwa maarufu zaidi nyimbo hiyo imezoeleka sana kama nyimbo ya Marijani, tatizo hilo pia liko katika nyimbo za Morogoro Jazz ambazo watunzi wake kama Mzee Mketema, kulwa Salum huwa hawatajwi kabisa na Mbaraka Mwinyshehe aliyekuwa , Kiongozi, mpiga solo na mwimbaji kuonekana ndie mwenye nyimbo.

Bila jina alisema ...

Heshima yako mkubwa!sasa mimi mbona ninaupande wingine wa historia kuhusu huo wimbo na bebdi nzima!in short nilinyoambia na mzee natdani utakuwa unamfahamu or ushamsika na yupo hapo kwenye picha Gordon alitunga wimbo huo,na mimi ni mtoto wake ambeye naitwa George,na mama yangu anaitwa Georgina

JFK alisema ...

ningefurahi sana tukiwasiliana maan unachosema kina maatokeo mengi, e mail yangu ni jkitime@gmail.com najua binti ya Jumanne alikuwa anatafuta haki za wimbo huu alipwe , hivyo ni muhimu nijue taarifa ya upande wako. Na kuongeza na wengine waliokuweko

Bila jina alisema ...

George,

Upo? Uko wapi? Msasani? Hatujaonana mika mingi sana. Mara ya mwisho tulionana Rose Garden miaka kadhaa iliyopita. Uncle Peter yupo? Naye nilionana naye miaka kadhaa iliyopita kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi(cheka)! Auntie Zoe na Sarah wapo? Nina hakika Siha amekuwa mtu mzima sana sasa. Wasalimie wote.

Mdau, Sokomoko Damu, Helsinki, Finland.