LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 2 Oktoba 2011

Muone Marijan Rajabu katika onyesho 'live'

Wengi humfahamu Marijani Rajabu kama mtunzi na muimbaji, lakini alikuwa pia mpiga gitaa mahiri, kama anavyoonekana katika video hii wakati yuko katika kundi lililokuwa na staili wakiiita 'Mahepe Ngoma ya Wajanja'. Hii ni clip fupi kati ya nyingi zitakazoonekana katika kipindi cha TV kitakachoanza kuwa hewani karibuni ili kuhifadhi historia ya sanaa zetu Tanzania.

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

Thanks Mwakitime for this wonderful clip.

seneta wa msondo alisema ...

uncle kitime i can't wait...kuhusu hiyo tv tunakuomba chonde chonde fanya uwezalo iwe inapatikana kwenye internet,wengine tuko ughaibuni na hatupendi kukosa uhondo huo utakao tusaidia pia kupunguza stress

seneta wa msondo alisema ...

Leo baada ya kuiona video hii nimeikumbuka kweli kariakoo yetu ya zamani..Doza alikuwa maarufu sana mitaa yetu ile,kila mtu alimpenda,nakumbuka mara nyingi nilikua nikienda pale mtaa wa somali kupiga nae stori tu marijani na mshkaji wake Abdul Salvador father kidevu,jamaa walikua marafiki sana toka wanasoma,marijani akiwa tambaza nadhani na salvador azania kama sikosei maana nilikua mdogo wao ni kaka zangu,ila nilikua nikimuona salvador akitoka kwao ilala anakuja taratibu na lindi street
anavuka uhuru anakuja somali kumpitia marijani hao mdogo mdogo kwa mguu wanaelekea shule kupitia mnazi moja wanaigia upanga,wanatokea muhimbili haoooo

sayz mdau wa us

Bila jina alisema ...

Ise nilikuwa sijui kama Marijari alikuwa anapiga solo! RIP

Bila jina alisema ...

Marijani alikuwa ni mkali wa kucharaza solo na ndio maana Dar International haikutetereka baada ya mpiga solo wake wa kutegemewa Mohamed Tungwa kutimkia Kenya mwaka 1983. Marijani alichukua jukumu la kupiga solo hadi hapo bendi iliposambaratika mwishoni mwa miaka ya 80. Solo la Marijani linasikika katika nyimbo kama Nyota Njema Imewaka (Jirani) na Dunia Imani Imekwisha.

Kacha Forlie alisema ...

Hakika haitakuwa vyema na haki kukushukuru Mkubwa Kitime kwa kazi nzuri hizi.Mtu kama Marijani Rajabu vijana wa rika langu husikia tu nyimbo zake yaani kumbukumbu ya sura yake haipo...God Bless you na uishi maisha marefu kwa kutuunzia,kuzienzi na kutuletea historia.
Great Job JFK.