LAPF

LAPF
LAPF

Jumamosi, 22 Oktoba 2011

Video ya Jerry Nashon na Vijana Jazz, Vijana Day-hebu angalia uchezaji wa wapenzi wa enzi hizo

Mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90, ungefika kuanzia saa nane mchana, siku ya Jumapili, katika Ukumbi wa Vijana Hostel (ukumbi unaopakana na Mango Garden), ungekuta vijana wameanza kukusanyika wakisubiri saa tisa mchana ambapo Vijana Jazz walikuwa wakianza muziki. Siku hiyo ilifahamika kama Vijana Day. Ungemkuta Mzee Jacob tayari mkali kabisa mlangoni akifukuza watoto wanaojaribu kupanda ukuta kuingia kwenye muziki. Kwa kweli waingiaji wa muziki walikuwa wengi kiasi cha kuweko milango miwili ya kuingilia. Na kama siku hiyo ni sikukuu basi ungekuta foleni imeshapangwa ya watoto, vijana na watu wazima wakingojea kukata tiketi za kuingia. Katika maktaba yangu nimepata bahati ya kukuta video hii ya onyesho live la Pambamoto. Ni video ambayo inaniletea masikitiko mengi kwani wenzangu wengi waliomo katika video hii wamekwisha tangulia mbele ya Haki. Pengine kwa wale waliokuwa wapenzi wa Vijana wakati huo watajiona katika kundi la wapenzi wa Pambamoto wanao onekana mwishoni mwa video hii. Hebu angalia staili za kucheza za enzi hizo  


Maoni 8 :

NN Mhango alisema ...

Zama hizo zilikuwa zama za dhahabu ikilinganishwa na sasa. Ingawa kila kizazi kina namna yake ya kufanya mambo, vijana wa sasa wanaojihusisha na muziki wanahitaji kufanya utafiti na ubunifu badala ya kudandia mila za wengine na kulewa usupa staa uchwara. Naipongeza blog hii kwa dhati kujaribu kurejesha historia kwenye njeo ya sasa.

Bila jina alisema ...

Pole sana kaka Kitime si wewe tu hata sisi tunaikumbuka vijana day ukiangalia list ya watu waliotangulia mbele ya haki ni wengi duniani tunapita tu. Mungu awalaze mahala pema peponi. Amina.

Perez alisema ...

"... subiri kidogo mamii, ae ae mama,
pesa bado zanisumbua ee mama, ae ae mama.."

..simbula simbulayoo simbula mamaa..

mnaukumbuka huo wimbo? nadhani unaitwa MWAMVUA.

we acha tu!

Bila jina alisema ...

Huyo jamaa anayepiga solo si Miraji Shakashia?

seneta wa msondo alisema ...

Du miraji shakashia enzi bado mdoooooogo.....watu tunatoka mbali jamani loh!mzee mzima mzee wa kazi kitime nakuona hapo...safi sana,namlilia jerry nashon bado

Bila jina alisema ...

Hivi jamani kuna bendi ambayo ilikuwa inapiga nyimbo ambazo vyombo, melody, sauti za waimbaji na ujumbe zipo well synchronised kama Tancut almus?Mimi nasema kama hii bendi ingekuwa makazi yake Dar isingekufa na ingepewa heshima yake kama bendi kali kuliko zote wakati ule. Najua wanamuziki wa bendi hii walienda Dar na kujiunga na bendi kama Maquiz, Vijana, Sambulumaa, Super matimila na nyinginezo ndo maana zikawika pia. Vijana ndugu yangu wa kwanza hapo juu wameharibikiwa. Mimi miaka hii ya 90 nilikuwa na miaka 10 kwaiyo naweza kujiita kijana. Lakini bado najua tofauti ya nyimbo kama Kashasha na zile za bongofleva. Nyimbo hata ingekuwa ya mapenzi ilikuwa inasababu yake na unaeleweka sio kuimba imba Baby gal in da house kwenye kila wimbo wakati hata kiingereza cha kuazima. Ipo siku nitarudi Tanzania niwashawishi vigogo wa CCM kwanza wairudishe Vijana Jazz na kushawishi ma-sponsor wawekeze kwenye muziki wa dansi wa ukweli acha izi Twanga pepeta na zinginezo zinazokopi kopi mahadhi. Halafu huyu Shakashia kumbe alikuwa mpigaji solo mzuri tu. Lini alianza kunakili solo za kikongo? Natamani nilie ngoja niache mie!

Bila jina alisema ...

Bwana Perez, kama sikosei wimbo huo uliotutajia hapo juu aliuimba Jerry Nashon wakati huo akiwa Bima Lee. Aliuimba na akina Athumani Momba (RIP). Solo alikung'uta Patrick Kamaley 'Bedui'.

severin mtitu alisema ...

Dah mjomba kitime....wakati umeenda sana.enzi hizo Dar inanukia na watu wanajuana....sifa kwako na mungu akupe maisha marefu tupate kuyqjua mengi kuhusu muziki wetu na kuwakumbuka wazee wetu waliotangulia mbele za haki.