LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 16 Januari 2012

Vicent Chopeta, mwanamuziki wa zamani wa The Strokers afariki dunia

Waliokaa toka kulia ni Marehemu Vicent Chotepa, wa pili ni Harry Chotepa
Vincent Chotepa,Mwanamuziki wa zamani wa The Strokers, bendi iliyokuwa na makao yake Upanga amefariki dunia katika hospital ya Muhimbili baada ya kufanyiwa operesheni ya sikio. Kwa maelezo ya jamaa zake wa karibu Vicent alikuwa mfamasia kwa miaka mingi pale Muhimbili na miaka ya karibuni alikuwa Ocean Road Hospital. Msiba uko Sinza mapambano, mazishi yanategemewa kuwa Jumatano tarehe 18 January 2012 baada ya kuwasili baba yake na dada zake waliokuwa mbali na Dar es Salaam.
Mungu amlaze pema peponi Amen

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Kwanza kabisa natoa pole kwa wafiwa wote waliowapoteza wapendwa wao katika habari za kusikitisha tulizozisoma hapa leo. Pia namwomba Muumba wetu awasamehe madhambi yao na kuwalaza pema peponi. Lastly, but not least, nampa ahsante J Kitime kwa (a) kutupasha hizi habari za kusikitisha na (b) kutukumbusha historia zao.

Bila jina alisema ...

Ooooh no! Not again!?

What happened recently with death?

Jamani! Mauti yamewatwaa ndugu, jamaa,marafiki na washirika wetu wapendwa wengi kwa nguvu sana siku za karibuni.

Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu Akumpumzishe kwa Amani Vincent. Amina.

Fidelis M Tungaraza.

Sam Mnkande alisema ...

Poleni sana John. Nilikuwa nafahamiana vizuri sana na Vincent, Harry na familia yote ya akina Chopeta. Familia zetu zilikuwa ni marafiki sana.

RIP Vincent