LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 17 Septemba 2012

MUZIKI WA TZ- MAONI YA WADAU


Kuna comments nyingi hutolewa kwenye blog baada ya kila post nimechagua baadhi tuzisome maana ni za walikuwepo na waliyoyakumbuka, kwa hiyo zina utamu wa pekee.................Pichani ni awamu ya kwanza ya Strokers. Waliosimama, Pino Makame, Freddie Lukindo, David Max. Waliokaa (?),Harry Chopeta, Vincet Chotepa.
Comments kuhusu picha hii
-Hebu angalia sign za vidole za Freddie, Bongo Flava take care hamjagundua kipya.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++Sam Mnkande said...
Kushoto ni Balozi Maharage,na kulia marehemu Herbert Lukindo, boy I remember those days


**************************************************************


Mkuu Mickey,

Cozzy Cafe Mkwepu na Makunganya Street Roundabout oppposite na Mbowe na Emms Hotel Independence Avenue, vipi? Dolphines Mkwepu Street na ile Tea Room ya Jamhuri na Mkwepu Street jina lake limenitoka. Kiambaza cha NBC City Drive Branch? Dengu Beach?

Forodhani Hotel, Afrosa wanajifua kuelekea Lagos, Nigeria Fiestac 77' au '78. Trippers inaanza kuyoyoma. Hizi ndiyo tunaweza kuhesabu zilikuwa dakika za majeruhi before things fall apart.

Babake TTC inaungurumisha mahoteli mijini, kanda za Bahari na nyikani. Grill Room kila hotel. Leta safu za mameneja kina Kibogoyo, Kadu, Njunwa, Kabendera, Tibenda, Ali Short naomba uendeleze ........, ......,

Shuttle inakubeba toka New Africa inakuacha Kunduchi Beach. Halafu inakubeba toka Kunduchi Beach inakurudisha New Africa.

Juhudi zako tu shule bure na kazi utapata! Balaa tupu, raha mtindo mmoja, hakuna kuchoka, hakuna stress. ukibamba yale mambo tetlacycline(njano na nyekundu) inamaliza mambo. Gnawing old dry bones is not good, mghh!?

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++nonymousFreddy Macha said...
Nakumbuka Groove Makers ilipoundwa...ilivuma kwa muda kisha ikanyauka. Tulikuwa na bendi kibao za vijana mjini baada ya mwana-Blues- Buddy Guy kuja Tanzania (1969). Sparks, Comets, Tonics, Afro 70, Barkeys (siku hizi Tanzanites), Sunburst, Rifters nk. Bahati mbaya enzi hizo hakukuwa na TV wala tasnia ya muziki kama ilivyo leo na Bongo Flava. Ingekuwa hivyo tungefika mbali. Ndiyo maana Blog lako John Kitime ni mwenge pekee unaomulika siku hizo...bila hivyo hakuna mtu angewakumbuka marehem Herbert Lukindo...na wengine wengi- Kassim Magati, James Mpungo, Choge Sly, nk

********************************** 

 
nonymousFreddy Macha said...
Habari nzuri...je Joseph Jengo yuko wapi siku hizi? Wakati akisoma Ilboru-(Arusha) alikuwa kaka yetu mkubwa na tulimpa jina la "mfalme wa Mabitoz."
Leo itakuwa kama mfalme wa "Masharobaro"
Nikiwa kidato cha kwanza (yeye ndo anamaliza cha nne 1969) tulikuwa tunamwiga mpaka vile anavyotembea. Alikuwa na kitu "staili"...


+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 nonymousAnonymous said...
Kusema ukweli bwana kitime sijui niseme nini au nianzihe wapi sabababu unikumbusha mblali na hiyo nyimbi niko nayo kwenye cd nakumbuka vizuri sana nyimbo hiyo irirudiwa upya uku ulaya na mzee koko kayinda mwanzilishi wa mangelepa akapiga tumba ni safi sana,mziki wa hawa wakongoman wa leo ni kelele tuu na wanapiga staili moja kama wera son jb mpiana au koffi au ferre gola zamani muziki wa kitanzania ulikuwa ni mtamu mno ukisikia bima lee ni moto na mziki wao no tofauti na wa msondo au sikinde au makassy au vijana jazz ,Tan cut alimasi,uda jazz band ,au jamuhuri jazaz au tabora jazz,oss bwana kitime hongeara kwa kazi ya kuelimisha jamaa kuhusu mziki wa Tanzania,leo hii utasikia eti akudo ndio wazee wa masauti sauti gani?ukisikia nyimbi za ddc za miaka ya 80 mpaka 95 hawa jamaaa hawifiki hata nusu au nyimbo za kina oss au maquiz au tan cut alimasi,au dr remmy ongara naomba watanzania tuanza kupenda vyetu ,ukienda congo autasikia wanapiga nyimbo za kiswahili au kuimba kiswahil naomba sana serikali iangalia sana kuhusu muziki unaopigwa tanzania kwenye radio asilimia 60 au 70 uwe mziki wakitanzania na wenye lugha ya kiswahili au mziki wa asili.Ezi za mwalimu rtd ndio alikuwa championi wa kupromoti muziki wa tanzania pia nyimbo za tanzania zifadhiwe kama hawa wenzetu wa uku,kwa mfano nyimbi za jimmy reeves,peter tosh.la mwisho naomba watanzania tuupende mziki wetu na lugha.
asante mzee kitime
yusef france

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
nonymousAnonymous said...
Ndugu Kitime,asante kwa kutupatia
uhondo na kutuamsha kutoka kwenye usingizi mzito ambapo habari nyingi kuhusu muziki wetu wa miaka michache tu iliyopita unaanza kusahaulika,matokeo yake watu wanashabikia mara Fm muzika mara akudo,kusema ukweli kama alivyosema mtoa maoni wa kwanza miziki hiyo ni makelele tu hata saauti za waimbaji hazina utamu wowote ukilinganisha na hao Simba Wanyika,Sikinde,OTTU,Dar int.Marquiz,Tancut,Dr.Remmy na bendi nyingi za zamani hakukuwa na makelele na kutaja majina ya watu mwanzo hadi mwisho.Hata tukirudi upande wa Congo pia akina Fraco,Tabu Ley,Pepa Kalle nk.waliimba nyimbo nzuri ingawa hatukuwa tunaelewa maana,na hawakuwa na makelele kama wakongo wa siku hizi.pia natoa ushauri wanamuziki wa ki tanzania tuache kuiga miziki ya aina hii na tuudumishe muziki wetu kama ulivyokuwa awali.Mini nilikuwa na hadi sasa ni mpenzi mkubwa wabendi ya Simba Wanyika kule Nairobi miaka hiyo,Pia mwana muziki mmoja kati ya hao Simba Wanyika Abbu Omar nilisoma nae Sekondari Songea Boys.naomba niwajulishe majina ya hawa wanamuziki kama waanavyoonekana kwenye hiyo cover ya Album yao.Juu toka kushoto ni George Peter,Joseph Just,Wilson Peter na chini toka kushoto ni JOhn
Olwenyo-rasta man(mkenya)Maneno Shabani(tangu enzi za Morogoro jazz)Abbu Omar,Prof.Jnr huyu Abbu Omar kwa sasa anafanya shughuli zake za muziki nchini Japan pamoja na Fresh Jumbe,hilo ndili kundi lililorudisha hadhi ya Simba Wanyika,baada ya Prof.Omari Shabani
kuchomoka na wanamuziki wote kwenda kuunda Les Wanyika.
J.Mdoe,Washington Dc.Usa.


*******************************************************

Ooo hoo hoho,
Sikujua kama utabadilika... x2

...Najuta kupoteza aa, wakati waangu, nyumbani kwako...,

...Baki salamaaa, kuonana nawe, ni majaliwa....,

Ooo hoo hoho,
Ulimwengu kweli una mambo mengii.

Yaani! We acha tu

****************************************
elete
nonymousAnonymous said...
Ukweli ni nikwamba muziki wa tanzania na congo unatokea kwa baba moja na mama moja ,cuba katika historia ya muziki wetu ni kwamba miaka 1930 mpaka 1940 Tanganyika ilikuwa na bendi za muziki wa dansi ambao ulikuwa ukipigwa kwa staili ya cuban chacha au rumba,muziki huu miaka nenda rudi ndio wakauperak mbele na kuanza kupiga swahili rumba sawa sawa na cuban rumba,ndio ukwa mwanzo wa au msingi wa muziki wa dansi na huu msingi tunao useema nikuanzia kwenye mpangilio wa vyombo na kwenye uimbaji pia,kwa mfano ukisikia nyimbo za Tanzania za zamani utasikia hakuna tofauti na nyimbo zilizokuwa zinapigwa na kina franco au tabu ley au wendo kolosy the GOD FATHER OF CONGOLIES RUMBA au Dr Niko,huu msingi uliendeleza muziki wa dansi ndio maaan ukisikia nyimbo za zamani za Tanzania ni tamu si kwa maneno tuu bali hata upiga wa vyombo au kuimba kwenyE key au note zile za kimuziki ni tofauti na leo kabisa wasomaji popete pale mlipo naomba msikia nyimboya ddc mlimani park ubaya ulianza zamani waimbaji wakiwa bitchuka, mzee wa busara mzee nguruma wakina mkanyia utasikia kweli hawa ni wanamuziki sio bongo flava au fm academia au nyimbo ya marehemu mbaraka mtaa wa saba alipiga gita ya soro katika mahazai ya jazz lakini akaifanya na stairi ya muziki wa dansi au sikiliza nyimbo ya mzee kiki jk kikwete au mimi na wewe tuu. kwa hiyo maoni yangu ni kwamba bwana kitime razima turudisishe azai ya muziki wa kiTanzania na siyo muziki wa kicongo man hatukatai muziki wa kicongo ila tuna taka muziki wa kitanzania uwe namba moja bendi zinazo piga muzuki wa kitanzania zipewe nafasi kubwa katika burudani muziki tz.
many thanks next time
yesf paris


+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
nonymousAnonymous said...
Kama sikosei, Rashid Hanzuruni (RIP) alikuwa M-TZ wa kwanza kupiga Hawaian guitar katika wimbo uliorekodiwa "usione nikiandamana, ukadhani nafuata bendera, napenda sana nchi yangu, shika moyo utakueleza, twende haya twende, tufurahi tukiandamana..." Kama nimekosea lyrics naomba nisahihishwe wazee...


nonymousAnonymous said...
Mkuu,

Kila nikitaka kuiburudisha nafsi yangu moja ya kisuuza nafsi yangu ni kibao cha Roza cha Western Jazz Band wana Saboso. Mama watoto wangu huwa akinikuta nasilikiza Roza huwa anajua leo Mzee kafurahi.

Zamani nilikuwa na kanda yake. Baadye nikaja kukipata katika CD ya The Most Beautiful Songs Of Africa.

Kibao cha Roza hata kama nina mambo gani yanayoniudhi nikikisikia huwa nafarijika sana. Huwa kinanikumbusha Dar ya miaka ya mwanzoni mwa sabini. Hunikumbusha mitaa ya Ndovu na Twiga, Jangwani. Hunikumbusha marafiki zangu wanandugu watatu mabaharia maarufu sana waliotokea mitaa ya Jangwani. Mmoja wa wanandugu hao nilikutane naye mara ya mwisho asubuhi moja mwaka 1997 karibu na mitaa ya Odeon Cinema akanizoa mpaka Mtaa wa Lumumba karibu na makao Makuu ya CCM akanilazimisha kunywa naye bia asubuhi subuhi ambayo si tabia yangu lakini kwa sababu ya urafiki wetu wa miaka mingi tangu shule ilinibidi ninywe naye.

Halafu nikikisiliza kibao cha Vigeregere kinanikumbusha sana The Tanzanites Band na yule mwimbaji wa Kisouth Africa, Thami The Dynamite enzi za Simba Grill, Kilimanjaro Hotel. Thami alikuwa akiimba ile nyimbo vizuri sana na The Tanzanites walikuwa wanaipigia backup nzuri mno. Nilikutana na Thami mara ya mwisho mjini Adelaide, Australia mwaka 2004 kwenye tamasha la Fringes WOMADELAIDE nikamuimbia Vigeregere akanidaka juu kwa juu akaanza kuuimba.

Asante sana.

Hakuna maoni: