LAPF

LAPF
LAPF

Jumapili, 21 Oktoba 2012

RIP MOHAMED IDD aka CONTROL


TANZIA, Mpiga gitaa mahiri MOHAMED IDD aka "CONTROL" amefariki dunia leo alfajiri. Wakati wa uhai wake marehemu amewahi kupigia bendi kadhaa zikiwemo Double O ya King Kiki,  National Panasonic, Mlimani Park, OTTU na alienda kufanya kazi Uarabuni na  Zanzibar Sound ya Asia Darwesh. Baada ya kukaa Uarabuni kwa muda aliamua kurejea bendi yake ya zamani ya Sikinde. Miongoni mwa vibao vilimpatia umaarufu ni pamoja na wimbo Gloria wa OTTU ambao alipiga solo. R.I.P IDD CONTROL

Maoni 1 :

Kisondella, A.A alisema ...

Thanks Bro JK for this Info

Nilimfahamu vizuri sana Mohamed Idd mara tu alipojiunga na Bendi ya Sikinde.

Mohamed Idd alikuwa na upigaji tofauti sana wa gita la kuongoza ukilinganishwa na wenzake kama Ramadhani Mapesa, Marehemu Kassim Rashid. Hivyo ilikuwa rahisi sana kwa mtu ambaye anayeufahamu muziki kujua huu wimbo nani anapiga solo.

Kama tunavyozungumza kila siku katika kuchangia kwenye hizi blog - tunapoteza watu muhimun katika upigaji wa muziki lakini warithi ni vigumu - kwa hili najua muziki wa Tanzania will declare at some moment of time dead - na hivyo tukajikuta woooooote tunaangalia Bongo Flava au Bongo Gospel

R.I.P Mohamed Idd - I will miss your wonderful gitar play