LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 25 Machi 2013

Marijani Rajabu alifariki 23 March 1995

Tarehe 23 March 1995, ndio siku ambapo Jabali la Muziki Marijani Rajabu alifariki kutokana na matatizo ya moyo kuwa mkubwa. Watanzania wakubwa kwa wadogo mpaka leo bado wanafaidi sauti ya Jabali hili, kuanzia nyimbo zake akiwa na STC Jazz Band kama vile Usiku wa manane, Shida, na nyingi mno akiwa Safari Trippers kama Georgina, au Siwema na Zuwena ambazo zilirudiwa na wanamuziki ambao hata hawakuwahi kumuona Marijani ni uthibitisho tosha kuwa Jabali au maarufu kwa rafiki zake kama Doza (kifupi cha Bulldozer kutokana kuwa bonge ya mtu). Siku za mwisho za maisha yake hazikuwa nzuri pamoja na kazi kubwa aliyoifanya katika historia ya muziki wa Tanzania. Siku za mwishoni alilazimika kufungua kajiduka akawa anauza kanda za nyimbo zake ili kujikimu. Mungu amlaze pema peponi.

Hakuna maoni: