LAPF

LAPF
LAPF

Jumanne, 30 Aprili 2013

VIDEO YA MAQUIS DU ZAIRE YA CHINYAMA , ENZI ZAO

Hawa ndio Maquis Du Zaire, wimbo huu, Kasongo, ulimletea matatizo sana King Kiki ambaye ndiye aliyeutunga, maana serikali yake ya Kongo wakati huo Zaire ikiwa chini ya Mobutu Sese Seko iliuchukulia kama ni fumbo fulani la kisiasa. Hii ilitokea kutokana na kuwa upande wa nchi anakotoka Kiki, kulikuwa na upinzani wa daima na serikali ya Mobutu, japo mwenyewe Kiki anadai wimbo huu haukuwa na uhusiano wowote na matatizo ya nchi yake.  -->
Hapa wanaonekana vigogo kama Chinyama Chiyaza (Baba yake Elly Chinyama), Adios, Viking Nguza, King King, Kanku Kelly, Banza Mchafu na nyota wengine wengi wa miaka hiyo. Mungu awalaze pema wote waliotangulia mbele ya haki


Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

Bravo Kitime. Tuwekee video nyingine zaidi kama hizi katika YouTube. Wewe ndiye tegemeo letu. Dah! Wajukuu wa Kiki na wanamuziki wengine tunaowaona hapa wanapaswa kuiona video hii.

Bila jina alisema ...

Safi Balozi. Tunataka kuona video kama hizi za bendi za Tanzania zipiga muziki live.

Bila jina alisema ...

Kitime,we ni basiiiii. Yaani mkuu, wewe ni zaidi ya balaaaa! Naenda kujifungia chumbani kulia.

John Kitime alisema ...

Mkuu kwanini ulie?

seneta wa msondo alisema ...

Nimekubali

Bila jina alisema ...

Mkuu kitime mimi ni kizazi cha sasas lakini Music wa dansi unanikuna sana, mpaka sasa hivi natoka kwenda kwenye live Band pale laprima na bar tofautitofauti ambazo wana Muziki wa Dansi wanapigi.

Kitime pls fanyeni mpango wa kuandaa concept mziki wa dansi na nyimbo za zamani zikapigwa.

siku hizi hakuna muziki, unakwenda dansi manaanza mpaka mnamaliza hujasikia sauti ya trampet!