LAPF

LAPF
LAPF

Alhamisi, 24 Julai 2014

ABBA KUNDI LA MUZIKI TOKA SWEDEN, LILILOWAHI KUTINGISHA DUNIAKundi la ABBA lilianza mwaka 1972, na lilikuwa ni la vijana wanne wa Kiswidi Agnetha Fältskog, Björn Ulvaeus, Benny Andersson, and Anni-Frid Lyngstad. Na kutokana na herufi za kwanza za majina yao ndio wakapata jina la kundi lao ABBA. Katika historia ya muziki wanasemekana ndilo kundi lililofanikiwa sana kibiashara kwa kuwa katika top ten ya mauzo katika nchi mbalimbali duniani kwa kipindi cha miaka 7 kati ya 1975 mpaka. Mwaka 1974 kundi hili ndipo lilipojitokeza kwa kushinda yale mashindano ya muziki wa nchi za Ulaya ya Eurovision Song Contest. Na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya shindano hilo kwa kundi toka Sweden kushinda,  na pia kwa mara ya kwanza Sweden kuwa na kundi ambalo lilikuja julikana dunia nzima. Kundi la ABBA liliuza zaidi ya album na singles milioni 380. Agnetha na Bjorn  walioana na pia Anni-Frid na Benny walikuwa ndani ya ndoa japo ndoa zote zilikuja vunjika.  Ndoa zao kufikia 1981 zilikuwa zimekwisha vunjika, tatizo kubwa ni kutokana na mzigo wa umaarufu.
Mwaka 1982 kundi lilivunjika japo haijawahi kutangazwa rasmi kuwa kundi lilivunjwa. Wanaume katika kundi hili waliendelea kuwa pamoja wakitunga nyimbo kwa ajili ya michezo ya jukwaani(musicals), wakati akina mama kila mmoja akaanza shughuli kivyake (solo), na umaarufu wa kundi ukaanza kushuka. Filamu ya Mama Mia iliyotoka 1999 ikiwa na nyimbo nyingi za ABBA ilitengenezwa baada ya mchezo wa kuigiza (musical), wenye jina hilo kupata umaarufu sana. Filamu hiyo ndiyo iliyoingiza pesa nyingi zaidi ya filamu nyingine nchini Uingereza kwa mwaka huo. Wimbo wa ABBA, Waterloo,  ambao ndio ulioweza kuwafanya washindi wa Eurovisiona Song Contest ulichaguliwa kuwa ndio wimbo bora uliowahi kutokea katika shindano hili.


Hakuna maoni: