LAPF

LAPF
LAPF

Jumatatu, 10 Novemba 2014

LEO NIMEKUMBUKA KIBAO MASAFA MAREFU CHA TANCUT ALMASI...angalia video


Kasaloo Kyanga ndie mtunzi wa kibao hiki maarufu, kilirekodiwa RTD Dar es Salaam katika awamu ya pili ya recording za Tancut Almasi. Recording hii ilitaka kuvunja bendi kwa kuwa wakati bendi ikiwa studio, Said Mabela alipita studio na Katibu wa bendi akamuuliza kwa siri anausikiaje muziki? Sijui kwa sababu gani lakini Mabela alijibu, "Hapa hakuna kitu nasikia solo tupu". Katibu wa bendi ambaye pia wakati huo alikuwa Katibu wa tawi la JUWATA la Tancut, akatujia juu wanamuziki wa Tancut kuwa tunapiga solo tupu na hivyo tuache kurekodi na bendi irudi Iringa kwa mazoezi zaidi. Ulikuwa ugomvi mkubwa, wakati huo Mabela amekwisha ondoka hata kumuuliza alikuwa ana maana gani haikuwezekana. Fundi wa RTD James Muhilu ndie aliyemtuliza Katibu huyo kwa kumueleza kuwa nae haelewi maana ya maneno ya Mabela na recording ikaendelea na dunia ikapata bahati ya kusikia kibao hiki. Nakumbuka katika awamu ya kwanza ya kurekodi Sidi Morris alikuja studio na kupiga tumba katika vibao kadhaa kikiwemo Wifi utunzi wa mwenye blog hii John Kitime. Hili lilileta mzozo Maquis ambako Sidi alikuwa akifanyia kazi na hivyo akasimamishwa bendi kwa kushiriki kurekodi

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Kitime naomba wimbo wa MTAULAGE MWANA.. sikumbuki uliimbwa na band gani kutoka mkoa wa Iringa, kati ya Tacut almas au Embakassy band (Mtandi) chini ya mzee wa sharubu.

Bila jina alisema ...

Kitime ni jambo Zuri kutengeneza Blog Kama hii inayohusu Wanamuziki wa miaka ya nyuma. Hebu tupe picha ya Tancut Almasi na Wanamuziki mliokuwa nao.